Shalom!,
UTII kwa kiingereza Obedience. Ni kufuata amri, ombi, au sheria au uwasilishaji kwa mamlaka ya mtu mwingine. Au mamlaka ya juu zaidi na kuyafuata pasipo kujali ama kuangalia linakubaliana na maamuzi yako ama linakinzana na maamuzi ama mawazo yako.
Lakini si kila jambo tunaloambiwa kutii tunafaa kulitii la! Hususani katika mambo yanayokinzana na imani yetu. Tutajifunza ni mambo yapi tunapaswa kutii na yapi hatupaswi kutii hata kama mamlaka yenye nguvu zaidi imeamuru.
Lakini tufahamu kuwa biblia inatutaka tuwatii watu wote.
JE! KUNA UTII WA NAMNA NGAPI?
upo utii wa namna mbali mbali kutokana na mazingira yetu yanatotuzunguka na watu tunaokaa nao tutakwenda kutazama moja baada ya nyingine.
- UTII KWA WAZAZI WETU.
Wakolosai 3:20 “Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana”
Neno la Mungu linatutaka kama watoto ambao tunao mama na Baba waliotuleta duniani na wametulea na kutukuza. Hili ni
Agizo la Mungu kuwa sisi kama watoto hatuna budi kuwatii wazazi wetu. Maana katika kuwatii ziko baraka nyingi na Neema pia pale tunapowatii wazazi wetu waliotuzaa.
Na hii ndio Amri pekee yenye Ahadi ya kuishi maisha marefu.
Kutoka 20:12 “Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.”
Pia Bwana wetu Yesu Kristo alikuwa akiwatii wazazi wake hakuwadharau ingali alikuwa ni Mungu katika Mwili aliwasikiliza wazazi wake na kuwatii. Ukisoma LUKA 2:51.
Utii wa kuwatii wazazi wetu ni kwa Faida Yetu wenyewe wala si kwa Faida ya Mungu. Maana biblia inatuambia “waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi……” hivyo hatupaswi kuwadharau haijalishi tunawazidi Elimu, Fedha nk tuwatii maana ni wazazi wetu.
2.UTII KWA WAZEE.
Jambo hili tunalisoma katika
1Petro 5:5 “Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu,..”
Pia Mungu ameagiza sisi Vijana tuwatii wazee wazee wa kanisa na walio katika kanisa, lakini pia wazee tunaoishi nao katika jamii yetu inayotuzunguka.
Wanapo tuelekeza ama kutuonya juu ya mambo fulani basi hatupaswi kujibizana nao ama kushindana nao kwa namna yoyote ile. Haijalishi umri wao umeenda vipi hatutakiwi kuwadharau tukifanya hivyo kamwe tusidhani Mungu yuko pamoja na sisi tukumbuke tumeambiwa “tuwatii” nasio kuwabeza.
1Timotheo 5:17 Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha
1Timotheo 5.1 Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na vijana kama ndugu;
Hivyo tusiwadharau kwa maarifa na nguvu tulizonazo kumbuka “Vijana tuna nguvu na speedi lakini njia wanazifahamu wazee”.
3.Utii kwa Mume.
Agizo hili wanawake/mabinti/wamama Mungu amewapa kuwatii waume zao katika kila hali ama kwa kila namna.
Pasipo kujibizana nao ama kuwadharau haijalishi wakoje!.
Tunalidhibitisha hilo katika..
1Petro 3:1 ” Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; ……5 Maana hivyo ndivyo
walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.
6 Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote”
Neno linatwambia “wanawake watakatifu wa zamani walimtumaini Mungu kwa kuwatii waume zao.”
Kama mwanamke ulieokoka hupaswi hata kidogo kumdharau mume wako haijalishi unakazi nzuri na mshahara mkubwa kuzidi yeye. Inakupaswa umtii haijalishi anamadhaifu mengi kiasi gani mtii muombee kwa Mungu hivi ndivyo inavyowafaa wanawake watakatifu kuwa.
Soma pia Wakolosai 3:18 jambo hili pia utaliona mtume Paulo akilizungumza kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
4.UTII KWA VIOGOZI WETU KATIKA IMANI.
Tunapaswa kuwatii viongozi wetu katika imani maana wao ndio wanaotuongoza wakipokea maagizo kutoka kwa Kristo Yesu alie kichwa cha kanisa hivyo tunapowadharau viongozi wetu katika imani moja kwa moja tunakuwa tunamdharau Kristo aliewaweka ili kutuongoza sisi.
Filemoni 1:21 “Kwa kuwa nakuamini kutii kwako ndiyo maana nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo”
Hata kama tunawazidi vipato na Elimu ndio Mungu amechagua watuongoze hatuna budi kuwatiii.
UTII KWA WAAJIRI WETU.
pia biblia inatutaka kuwatii waajili wetu,ama mabwana zetu wanapotupa maagizo ya kufanya.
Haijalishi umeokoka na unasikia sauti ya Mungu wazi wazi na kuzungumza nae kama Musa usipomtii Bosi wazi usidhani Mungu atasimama upande wako. Jua kabisa utafukuzwa kazi. Hivyoo watii. Katika mambo yasioenda kinyume na imani yako.
Waefeso 6:5 “Enyi watumwa, watiini wao
walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo;
6 wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekazao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo;
7 kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu;
8 mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru.”
UTII KWA WENYE MAMLAKA.
Kila mamlaka iliyopo chini ya jua katika kila nchi vyombo vya usalama,Maraisi, wabunge nk wote wanafanya kazi za Mungu na Mungu ameridhia wawepo. Lakini kama serikali inasema usipokee rushwa,nk na ukapokea ukakamatwa usizani kuwa Mungu atakutetea haijalishi utaomba mara ngapi maadamu haukitii mamlaka na Sheria iko kwa ajili ya kukushughulikia na utatumikia adhabu hivyo kile mamlaka ilichoagiza tii.
Kama ni kulipa kodi lipa kwa uaminifu, kama mwisho kutembea ni saa6 usiku kwa sababu za kiusalama tii kaa nyumbani kwako.
Tito 3:1 “Uwakumbushe watu kunyenyekea
kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema; 2 wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote.
- UTII KWA MUMGU WETU.
Utii wenye nguvu na mamlaka ambao tunastahili kuutii hata ni kimyume na viongozi wetu ni Kumtii Mungu kwani yeye ndio aliejuu kuliko wote.wala HAKOSEI huu ndio utii wa juu sana kuliko mwingine.
Maana katika kumtii Mungu Kuna nguvu kubwa na umuhimu mkubwa sana soma Yakobo 4:7.
Tusome pia…
Wafilipi 2:7 “bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa MTII hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; 11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
Pia anaendelea kusema katika.
Waebrania 5:7 Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;
8 na, INGAWA NI MWANA, ALIJIFUNZA KUTII kwa mateso hayo yaliyompata;
9 naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;
Na sisi kama watoto wa Mungu tuliokombolewa na damu ya Kristo Yesu hatuna budi kutii kama Bwana wetu alivyotii ingali alikuwa ni Mungu katika mwili(Emmanuel)
JE! UNAPASWA KUWATII WATU WOTE HATAKAMA KILE WANACHOKUAMBIA KINAKINZANA NA MUNGU?.
Biblia inatuambia hatupaswii kutii maagizo yotote yanayokinzana na Neno la Mungu hata kama ni nani kasema ni sharti tumsilize Mungu na tumtii yeye kwanza.
Kama vile mitume Petro na Yohana walizuiliwa kuhubili injili lakini ni kipi walichosema”je inatupaswa kuwatii nyinyi tusimtii Mungu?”
Tusome
Matendo 5:27 “Walipowaleta, wakawaweka
katika baraza. Kuhani Mkuu akawauliza,
28 akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu.
29 Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu”
WAZAZI.
ikiwa wazazi wako wanakwambia kufanya matambiko,kufanya ibada za wafu,kwenda kwa waganga,kuridhishwa uchawi nk. Hupaswi kuwatii na jambo hili si dhambi kabisa usipowatii mbele za Mungu bali utaonekana mtu unaejitambua.
SERIKALI.
Hupaswi kuitii pale inapoweza zuio la wewe Usimuabudu Mungu wako ama kufanya ibada. Usaini mikataba ya Rushwa ama madawa ya kulevya ama bidhaa mbovu mamlaka inakutaka ufanye hivyo usifanye.
Kama vile Daniel ambavyo hakutii mamlaka ya ufalme wa Babeli hata kama Mungu ndio ameagiza tufanye hivyo usifanye kabisa mtii Mungu fanya ibada.
Na Mungu atakuwa upande wako kama vile Alivyokuwa upande wa Danieli.
MUME.
ikiwa mume wako anakulazimisha kufanya mambo yaliyokimyume na Neno la Mungu kama vile kutazama picha za uchi ili mfanye tendo la ndoa ama kutaka kukuingilia kinyume na maumbile kataa kabisa hutakiwi kumtii.
Utiifu wote ni lazima usikinzane na Neno la Mungu lakini ikiwa unakinzana na Neno basi usitii kabisa. Lakini ikiwa kwa mambo mengine ambayo hayaadhiri misingi ya imani yako kwa Mungu wetu, yaani Bwana wetu Yesu Kristo tii, bila kiburi kabisa.
Maana kinyume na hapo katika siku za Mwisho ibilisi kama ilivyotabiliwa kuwa .
2 Timotheo 3:1 Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
2 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, WASIOTII WAZAZI WAO, wasio na shukrani, wasio safi.
Ubarikiwe sana.
Jiunge na channel hii kwa Mafundisho zaidi
NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako piga namba hii 0789001312.