Nini maana ya RHEMA?

Uncategorized No Comments

Bwana Yesu asifiwe ndugu katika Kristo Yesu.

Katika Agano jipya biblia imeandikwa kwa Lugha ya kiyunani yaani Kigiriki. Na kutafasiriwa kwa lugha mbali mbali!, Sasa katika Lugha Yetu ya Kiswahili Neno la Mungu linatajwa katika sehemu nyingi kama “NENO “. sehemu nyingi tunasoma utakua “Neno la Bwana likanijia/Neno la Bwana likamjia”

Hivyo tunaliona katika sura moja peke yake. Sasa tukirudi katika Lugha mama yaani Kiyunani(kigiriki) Neno la Mungu limetumika katika maeneo makuu mawili.

Yaani Neno la wakati huo lakini pia Neno la Wakati wote yaani la Daima. Maneno haya ni RHEMA pamoja na LOGOS katika biblia ya kiyunani mahali Neno la Bwana likija basi lilikuwa likiegemea katika sehemu hizi mbili tutajifunza maane zake hapa.

LOGOS. Ni Neno la Mungu la wakati wote/daima litakalotumika vizazi na vizazi. Au tunaweza kusema mpango mkamilifu wa Mungu juu ya Mwanadamu juu ya ukombozi wetu.

Kama vile Bwana Yesu Kristo (Neno lililofanyika kuwa mwili).

Ni Neno linalotumika muda wote.

RHEMA . Ni Neno ambalo Mungu analitoa kwa wakati husika tu na baada ya hapo halitumiki tena. Kama Neno lililomjia Elisha kumwambia Jemedali yule Naamani kujichovya katika mto wa Yordani mara saba kisha atapokea uponyaji.

Hilo lilikuwa ni Neno la Wakati ule ili kutimiliza kusudi kwa wakati ule (RHEMA).

Mfano wa maandiko ya daima (LOGOS) unaweza kusoma

Yohana 1:1-18, Yakobo 1:22, Waebrania 4:12.

Lakini Rhema tunasoma mfano wake katika

Mathayo 4:3-4″[3]Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. [4]Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.”

Hivyo tunaweza kusema Biblia Takatifu yote ni LOGOS na Rhema ni Neno ambalo mtu anapewa kwa kipindi fulani ili kutimiliza kusudi ama jambo Fulani.

MUNGU BADO ANASEMA NA SISI KWA NENO LA WAKATI (RHEMA)?.

Ndio Mungu anasema na sisi kupitia Neno lake lakini pia anatupa Neno la wakati yaani Rhema ili kutimiliza kusudi fulani katika maisha ama katika kusudi lake yeye.

Tunapokuwa kwenye makusanyiko mbali mbali kwa ajiri ya jina lake iwe ni Ibada,Mikesha,mifungo,nk Mungu husema nasi Neno lake la wakati kupitia Maono, Unabii,Neno la hekima,Neno la Faraja. Kwa wakati huo ambao yeye anataka kutuwasilishia ujumbe wake.

Jambo la muhimu, kutambua Neno ambalo litafunuliwa ni lazima lisikinzane na maandiko matakatifu yaani Biblia. Yote kwq pamoja yasipokinzana yanatufanya tumuone na kumuelewa Mungu katika ukamilifu wote.

Sasa katika nyakati hizi za Mwisho wakati mwingine ni kukosa maarifa ama wanafanya kwa kujua kabisa ni kulitumia Neno Rhema(Neno la wakati fulani ili kutimiliza jambo fulani) wanalifanya kuwa ndio Neno la daima yaani (LOGOS) jambo ambalo ni hatari sana ni nyakati za kuwa makini sana. Wanashindwa kufahamu Neno lile lilikuwa ni wakati fulani kutimiliza jambo ambalo Mungu amekusudia.

Kama vile wana wa Israeli walivyoambiwa wamtaze yule nyoka wa Shaba Jangwani atakaeamini kwa wakati ule atapona.  Lakini utaona walienda nalo bila kujua mwisho wa siku Mungu akawaadhibu kwa kufanya machukizo ya kuendelea kuwa na yule nyoka hata walipotoka Jangwani.

Walishindwa kuelewa lile Neno lilikuwa ni la wakati ule.

Hivyo mwisho wa siku inageuka kuwa ni ibada ya sanamu, jambo ambalo ni hatari kubwa sana katika roho.

LOGOS (Neno la daima) ni Kristo Yesu ndio inabidi tutembee nalo wakati wote ule hata tutakapo ondoka hapa tutazidi kuwa nalo.

Tumtazame Kristo wakati wote.

Maranatha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *