Agano la chumvi kibiblia lipoje sawasawa na 2Nyakati 13:5

  Maswali ya Biblia


JIBU:

2Nyakati 13:5 “Je! Haikuwapasa kujua ya kwamba Bwana, Mungu wa Israeli, alimpa Daudi ufalme juu ya Israeli milele, yeye na wanawe kwa AGANO LA CHUMVI”

Katika Biblia neno ‘Agano la chumvi’ tunaliona mara tatu katika vitabu tofauti tofauti 2Nyakati 13:5,Hesabu 18:19 na Walawi 2:13.

Zamani na hata hivi leo katika baadhi ya jamii chumvi imekuwa ikitumika kuleta ladha ya chakula lakini pia inatumika kama kiungo cha kuhifadhi chakula kwa muda mrefu ili kisiharibike..


Chumvi ilitumika kuhifadhi chakula ambacho hakijapikwa(kibichi/kikavu) wakati ambapo hakukuwa na friji. Hivyo chumvi inalo Agano bora la kutunza kitu na kikadumu kwa muda mrefu bila kuharibika, ni kiungo pekee kinachoweza kufanya hivyo..

Tukiangalia hata kipindi cha Agano la kale tunaona wana wa Israel walipokuwa wakitoa sadaka zao za unga au za wanyama waliziwekea chumvi ili kuwakilisha agano bora la Mungu.


Mambo ya Walawi 2:13[13]Tena, kila toleo la sadaka yako ya unga utalitia chumvi; wala usiiache sadaka yako ya unga kupungukiwa na chumvi ya agano la Mungu wako; utatoa chumvi pamoja na matoleo yako yote.


Ezekieli 43:22-24[22]Na siku ya pili utamtoa beberu mkamilifu awe sadaka ya dhambi; nao wataisafisha madhabahu, kama walivyoisafisha kwa ng’ombe huyo.

[23]Utakapokwisha kuitakasa, utatoa ng’ombe mume mchanga mkamilifu, na kondoo mume wa kundini mkamilifu.

[24]Nawe utawaleta karibu mbele za BWANA, na makuhani watamwaga chumvi juu yao, nao watawatoa wawe sadaka za kuteketezwa kwa BWANA..

Kitu kilichotiwa chumvi kilidumu muda mrefu, na kudumu huko kwa muda mrefu inamaanisha kimetiwa chumvi nyingi Kuna usemi usemao wakongwe ni watu waliokula chumvi nyingi. Usemi huu upo pia katika maandiko ukisema wakongwe ni watu wenye chumvi mwilini..


Ezra 4:11-14[11]Hii ndiyo nakili ya waraka waliyompelekea mfalme Artashasta; Watumishi wako, watu walio ng’ambo ya Mto; wakadhalika.

[12]Ijulikane kwa mfalme ya kuwa Wayahudi, waliokwea kutoka kwako, wamefika kwetu Yerusalemu; nao wanaujenga ule mji mwasi, mbaya; wamemaliza kuta zake, na kuitengeneza misingi yake.

[13]Basi, ijulikane kwa mfalme, ya kuwa mji huu ukijengwa, na kuta zake zikimalizika, hawatatoa kodi, wala ada, wala ushuru, na mwisho wake wafalme watapata hasara.

[14]Na sisi, kwa kuwa tunakula chumvi ya nyumba ya mfalme, wala si wajibu wetu kumwona mfalme akivunjiwa heshima, basi tumetuma watu na kumwarifu mfalme..


Tunaona kwenye kitabu cha Mambo ya 2Nyakati 13:5,

2Nyakati 13:5 unaosema “Je! Haikuwapasa kujua ya kwamba Bwana, Mungu wa Israeli, alimpa Daudi ufalme juu ya Israeli milele, yeye na wanawe kwa AGANO LA CHUMVI”..

Hii ina maanisha kwamba Mungu aliingia kwenye agano na Daudi ili ampatie ufalme, agano hilo lilikuwa la kudumu kwa muda mrefu yaani ni kama chumvi inavyowekwa katika chakula fulani ili kidumu kwa kipindi kirefu..

Pale tunapoamwamini Yesu, tukatubu na kuziacha dhambi zetu TUNATIWA CHUMVI katika roho zetu ili tudumu milele katika uwepo wa Mungu na kisha kupata uzima wa milele…


SASA TUNATIWAJE CHUMVI ILI TUURITHI UZIMA WA MILELE


Jibu ni kuwa tunatiwa chumvi kwa MOTO

Marko 9:49 “Kwa sababu kila mtu atatiwa chumvi kwa moto”.


Moto huo ni ule wa Roho mtakatifu, soma Mathayo 3:11, Matendo 2:3

Huu moto wa Roho Mtakatifu unaposhuka ndani ya mtu unaunguza mambo yote yasipompendeza Mungu, na kumsafisha mfano wa chuma kinavyosafishwa katika moto. Hivyo moto huo unamtenga mbali na yale yote aliyokuwa ameshikamana nayo, maumivu yanaweza kutokea kwa sababu moto huo unaondoa viungo vyote vilivyokuwa vikimkosesha na kisha anakuwa kiumbe kipya na uzima wa milele unakuwa ndani yake, na hilo ndilo agano la chumvi kwa wale waliompokea Kristo.

Ndugu umetiwa chumvi au bado? Ikiwa utamkubali Kristo, Roho Mtakatifu atakutia chumvi na utaenda kuwa chumvi ya ulimwengu (Mathayo 5:13) na kupata uzima wa milele.

         Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT