Basi wamwitaje yeye wasiyemwamini?

Biblia kwa kina, Uncategorized No Comments

Bwana Yesu asifiwe ndugu yangu mpendwa katika Bwana, karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya Bwana wetu Yesu kristo maana yeye ndiye neno la Mungu kama maandiko yanavyosema 

Ufunuo 19:13   Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, NENO LA MUNGU. 

Maandiko yanasema kuwa kila atakayeliita jina la Bwana ataokoka, ni kweli kabisa, kila atakayeliita jina hilo ataokoka

Warumi 10:13  kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. 

Lakini watu wengi wanashindwa kuelewa kuwa, kama HUJAMWAMINI huwezi okoka siku utakapoliita jina hilo. Sasa kuamini haina maana kumkiri na kubatizwa tu na kisha kuendelea na maisha yako.

Kwa mfano: Mtu anakwambia kuwa, hiyo njia hapo si salama usipite, labda kuna wanyanganyi wabaya ambao wanaweza hata kupoteza maisha yako, lakini wewe ukamwitikia tu huyo mtu kuwa “sawa nimeelewa” lakini wewe ukapita hiyo njia na madhara ya wanyanganyi yakakupata. Sasa huyo mtu HAKUAMINI hayo maneno ya tahadhari aliyopewa, kwasababu kama angeamini ni wazi kuwa ile njia asingeipita.

Sasa wakristo wengi leo hii wanasema kuwa, wamemwamini Bwana Yesu kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yao, lakini ukichunguza kwa makini si kweli, kwasababu kuna vitu vingi sana ambavyo Bwana alisema kuwa, kama wakristo tuapaswa kuviacha na kutokuvifanya lakini watu bado wanavifanya, hivyo basi, wakristo wa namna hii ni wazi kuwa hawajamwamini Bwana  na ile siku watakapoliita hilo jina HAWATAOKOA kwani maandiko yanasema utamwitaje usimwamini?

Warumi 10:14   Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini?……………..

Umeona hapo Ndugu yangu? Wewe unayesema kuwa umeokoka na kumwamini Bwana, unatakiwa uamini neno lake kuwa, uache huo uzinzi unaofanya lakini kama hutaki kuucha fahamu kuwa bado hujamwamini na ile siku utakapoliita jina lake huko kuzimu fahamu kuwa hutaokoka huko.

Dada yangu unayesema kuwa umemwamini Bwana Yesu lakini hutaki kuamini neno lake linalosema kuwa, uvae mavazi ya kujisitiri na uache kuvaa hivyo vimini vyako na masuruali mtaani na Kanisani, kutwa kuwafanya wanaume wazini mioyoni mwao kwa kukutamani wewe, fahamu kuwa bado hujamwamini na huwezi okoka siku ile kwani utamwitaje yeye usiyemwamini?

Wewe unayesema umemwamini Bwana na huku hutaki kuamini neno lake kuwa usichukue wala kutoa rushwa, fahamu kuwa hujamwamini bado hivyo hata ukiita hilo jina hutookoka.

Mkristo unayesema kuwa umemwamini Bwana na huku hutaki kuamini neno lake kuwa uache kuabudu hizo sanamu, na kuwaomba hao wafu, fahamu kuwa wewe bado hujamwamini ndugu yangu na wala hutooka wala ibilisi asikudanganye.

Baba unayesema umemwamini Bwana, lakini hutaki kuamini neno lake kuwa uache pombe kwani walevi wote hawatourithi ufalme wa Bwana Yesu, fahamu kuwa hujamwamini na hutookoka siku ile. Maana yeye mwenyewe alisema kuwa, hatoitika kwasababu utakua umebatilisha shauri lake la kuacha hivyo vitu 

Mithali 1:25 Bali mmebatilisha shauri langu, Wala hamkutaka maonyo yangu; 

26 Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu, Nitadhihaki hofu yenu ifikapo;

27 Hofu yenu ifikapo kama tufani, Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli, Dhiki na taabu zitakapowafikia. 

28 Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika; Watanitafuta kwa bidii, wasinione. 

Umeona hapo? Bwana anasema kuwa, utamuita lakini hatoitika kabisa, hivyo ndugu yangu, tubia leo hayo matendo yako maovu unayoyafanya na wala usijifari kuwa  umeshamwamini Bwana na kubatizwa na huku hutaki kuamini maneno yake yanayosema uache uzinzi, pombe, sigara, matusi, uongo, uvaaji wa suruali na vimini, rushwa, make up, kujichubua, ibada za sanamu n.k Hutaki kuamini maneno ya Bwana na maagizo yake aliyoagiza tuyafanye kama vile kushiriki meza ya Bwana, kutawadhana miguu na wanawake kufunika vichwa wakati wa ibada. Fahamu kuwa, watakaookoka ni wale walio mwamini Bwana na maneno yake. Hivyo fanya leo uamuzi sahihi ili ukapate kuokoka siku ile utakapomwita.

Na kama bado hujampokea Bwana Yesu fahamu nafasi uliyonayo ni sasa na wala si baadae, wala kesho, hivyo tubu na ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kimaandiko.

Bwana akubariki. Shalom 


Mada zinginezo:

JIANGALIENI BASI JINSI MSIKIAVYO.


Je! Nikiwa naona maono si ndo basi Roho mtakatifu ninaye hivyo sina haja ya ubatizo?


TAFAKARI KWA KINA HATIMA YA UNACHOKIFANYA ILI MUNGU ASEME NA WEWE.


JINSI AMRI YA UPENDO INAVYOWAFANYA WATU WADUMU KATIKA DHAMBI


Je! Tunapaswa kushika sabato kulingana na Isaya 66:23?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *