fahamu maana ya kumbukumbu 22:7 sharti umwache yule koo aende zake, lakini makinda waweza kuyatwaa uwe nayo.

Biblia kwa kina No Comments

Bwana Yesu asifiwe,  Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tujifunze maneno ya uzima.

Kuna jambo kubwa sana ambalo Mungu alikuwa akiwafundisha wana wa Israeli nyuma ya hili andiko,
Na kwa neema za Bwana tutakwenda kuona na sisi kujifunza pia.

kumbukumbu 22:6-7
 6“Kiota cha ndege kikitukia kuwa mbele yako njiani, katika mti wo wote, au chini, chenye makinda au mayai, naye koo ameatamia juu ya makinda, au juu ya mayai, usimtwae yule koo pamoja na makinda; 

7 sharti umwache yule koo aende zake, lakini makinda waweza kuyatwaa uwe nayo; ili upate kufanikiwa, ufanye siku zako kuwa nyingi”.

Mungu aliwapa agizo wana wa Israeli kama mtu akiwa katika kutembea huku na kule akakutana na kiota cha ndege  koo kipo karibu kiasi kwamba anaweza akafanya lolote kwa muda mfupi na akafanikiwa pasipo kutumia muda mwingi wala nguvu na akili nyimgi pia. Walipewa sharti wasiwe na tamaa na wakawachukua wote.

Ila wamwache koo anende zake ili aendeleze uzao ila wale makinda wa koo wanaweza kuwachukua na kuwamiliki yaani kuwafanya wake.

Kwa kitendo kama hicho tu mtu huyo aliefanya hivyo anakuwa ameongeza siku zake za kuishi.

TUNAJIFUNZA NINI KATIKA MAISHA NA KATIKA UKRISTO?

1. KATIKA UKRISTO.

Katika nyakati hizi za Mwisho ipo mikusanyiko mimgi Sana,Kuna makanisa mengi na watumishi wengi sana pia lakini sio kila kanisa/huduma zinawaweka watu katika mstari wa wokovu ili waweze kusimama na kuyafahamu mapenzi ya Mungu ya kweli ni yapi na kuyafata.

Maana viongozi wao ni vipofu kama vile Bwana Yesu alivyosema kipofu akimuomgoza kipofu mwenzake ni lazima watatumbukia katika shimo wote.

Hivyo hakuna namna kiongozi akawa kipofu wale anaowangoza na wanamfata wakawa sio vipofu.

Sawa ikiwa wewe ni Mkristo ama mchungaji, nabii nk unayeijua kweli na ukaona kabisa watu fulani wapo katika upofu(mafundisho yasiyo imara/uongo) unaona kabisa mahali alipo anapotezwa usiache tu na kupotezea na kusema shauri yao ama sio washirika wako ama sio washirika wenzangu.

Lakini inapaswa uwaeleze ukweli uwaambie ilio kweli na kuwatoa hao ili uweza kuokoa roho zao.

Si rahisi kumgeuza kiongozi(inawzekana ikawa ni changamoto) huenda ukashindwa kumfikia ila wale washirikishe (makinda) huna budi
Kuwaelekeza katika njia ambayo ni sahihi. Kwa kufanya jambo kama hilo unakuwa umejiongezea baraka nyingi kutoka kwa Bwana.

Hivyo katika siku za Mwisho hizi watu wengi sana wameshikwa kwenye vifungo vya dini lakini ndani yao hakuna Kristo bali Kuna dini tu.

2.KATIKA MAISHA.

Katika maisha yetu tunazungukwa na watu wa namna mbali mbali moja wapo ni wapitaji kama vile mayatima, watu wasiojiweza kabisa hata kulisha familia zao hata kuwagharamia tu watoto wao, watu ambao hata kula kwao ni muujiza. Lakini tunapita kama hatuwaoni, kwa sababu tu sio ndugu zetu au watoto wetu.

Lakini Bwana anatupa ushauri ulio bora kama tukiuchukua kamwe hatutakuwa na majuto yoyote yale. Ni heri usiwajali wale wazazi lakini fanya juu chini wajali wale watoto wao utakuwa umeongeza siku zako za kuishi. Tofauti na inavyodhaniwa kuwa kuwaheshimu wazazi tu basi inatosha ni kweli lakini unapowajali na watoto wasiojiweza unazidi kujiwekea na kujiongezea daraja kubwa sana.

Tuyatafakari haya na tuenende nayo Bwana atatubariki hakika na kutuongeza sana.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *