HIRIMU NI NINI KIBIBLIA?

  Mitihani ya Biblia

Hirimu ni nini sawa sawa na andiko la (wagalatia 1:14)

Hirimu inamaanisha mtu aliye katika kundi la umri wako yaani rika lako
Mfano tunaposema Yohana na Petro ni hirimu moja, tunamaanisha Petro na Yohana ni watu mwenye rika moja (umri mmoja)

Lakini kibiblia neno hili hirimu linatafsirika kwa kina zaidi, maana mahali pengine linamaanisha kijana mdogo.

Mfano vifungu hivi vinazungumzia hirimu kama mtu wa umri mmoja na mtu mwingine

Danieli 1:10
[10]Mkuu wa matowashi akamwambia Danieli, Mimi namwogopa bwana wangu, mfalme, aliyewaagizia ninyi chakula chenu na kinywaji chenu; kwa nini azione nyuso zenu kuwa hazipendezi kama nyuso za vijana hirimu zenu? Basi kwa kufanya hivyo mtahatirisha kichwa changu mbele ya mfalme.

Hapa tunaona baada ya akina danieli kukataa kula vyakula vile, huyo mwangalizi wa vijana, towashi aliwaeleza wakina danieli, jinsi anavyoogopa juu ya kukunjamana sura zao, wakati vijana wenzao rika lao, watakapoitwa na mfalme wale wataonekana wamenawiri kuzidi wao

Ukisoma tena

Wagalatia 1:14-15
[14]Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu.
.
[15]Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake,

Hapo pia mtume Paulo anaeleza jinsi alivyokuwa na juhudi katika kushika dini za wayahudi, kuliko hata watu ambao alikuwa hirimu nao ,yaani umri mmoja na vijana wenzake

Lakini mistari hii, inataja neno hili, vikimaanisha kijana mdogo

Waamuzi 8:14
[14]Ndipo akamshika mtu mmoja hirimu katika watu wa Sukothi, akamwuliza; naye akamwandikia majina ya hao wakuu wa Sukothi, na wazee wa mji, watu sabini na saba.

Ukisoma pia waamuzi 17:7-11, 18:3

Sasa ni nini tunaweza kujifunza kutoka katika neno hili..?

Ikiwa na sisi tupo katika marika, je katika marika haya tuliyopo ni vitu gani vya maana tunafanya kwa Mungu wetu, mfano upo katika rika la miaka 12 jitathimini kwa kulinganisha na watu walio katika biblia walio kuwa na rika hilo, bidii yao mbele za Mungu ipo sawa na wewe, tunaweza jifunza hili kwa Bwana wetu Yesu kipindi yupo kwenye rika hilo alikuwa anashinda hekaluni akijifunza sheria ya Mungu, je na wewe rika lako hilo unalitumiaje je unafanya hivyo?

Mfano unakuwa katika rika la miaka 20, 25, 30 hadi 70


Je katika rika hilo ulilo nalo unalitumia namna gani


Je mambo ya dunia ndiyo kipaumbele kwako, ulevi, uzinzi, wizi nk..
Ikiwa bado upo katika hali hizo jua kabisa utumii vyema mda wako wa umri wako maana kumbuka hakuna anayejua kesho yake, hivyo ingekuwa ni heri ukijikita kuyatenda mapenzi ya muumba wako mfano kama kina Ibrahimu, Musa, Elia, Yusufu, Daudi hawa ni watu ambayo walitumia vizuri mda wao katika kumwakilisha Mungu katika maisha yao

Neno la Mungu linasema

Mhubiri 12:1-2

[1]Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako,
Kabla hazijaja siku zilizo mbaya,
Wala haijakaribia miaka utakaposema,
Mimi sina furaha katika hiyo.

[2]Kabla jua, na nuru, na mwezi,
Na nyota, havijatiwa giza;
Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua;

Uheshimu mda uliopewa na Mungu, heshimu umri wako usifanye mambo ambayo hata mbele za watu yanawasikitisha, thamini nafasi ambayo Mungu amekupa leo

Ikiwa bado ujaokoka na unatamani, leo uanze upya maisha yako, uutumie vyema umri kwa Bwana basi mlango uko wazi Yesu yupo tayari kukupokea wewe mwamnini, na umkiri kwa kinywa chako naye atakuokoa

Mungu akubariki

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10


Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kwa namba hizi
+225693036618/ +225789001312

LEAVE A COMMENT