KUJUZU NI NINI?

  Mitihani ya Biblia

Neno kujuzu maana yake ni “kutoruhusiwa”.

Tusome
2Wakorintho 12:2 “ Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu


3 Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua


4 ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene”

Paulo anaeleza maono aliyoyaona katika mbingu ya tatu, ambapo alisikia maneno yasiyotamkika ambayo hayaruhusiwi kwa mwanadamu kusema.

Neno hilo pia tunalisoma katika kitabu cha Mwanzo..


Mwanzo 34: 7 “Wanawe Yakobo waliposikia hayo, wakaja kutoka nyikani; nao wakasikitika sana, wakakasirika mno, kwa sababu amefanya upumbavu katika Israeli kwa kulala na binti Yakobo, neno LISILOJUZU kutendeka”

ambapo wana wa Yakobo walihuzunika na kukasirika waliposikia haya, kwani walikuwa wamefanya upumbavu katika Israeli kwa kulala na binti wa Yakobo.

Wakristo waliookoka hawaruhusiwi kuupenda ulimwengu, kuishi maisha ya dhambi na anasa, kuwa mtukanaji, mwizi, walaghai, mzinzi, mlevi, au kujifunga na watu wasioamini. Wanapaswa kujitahidi kwa ajili ya usafi na utakatifu, kuchukua msalaba, na kumfuata Yesu kila siku katika maisha yao. Biblia inasema bila utakatifu hakuna mtu atakayemwona Mungu.

Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”.


Kama ujampokea Kristo(kuokoka) Ni wakati wako huu,Usingoje Wala badae, Maaandiko yanasema saa ya Wokovu ni sasa..
wasiliana nasi kwa namba hizi: +255693036618 au +255789001312.

Jiunge na chanel hi kwa kubofya hapa

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

LEAVE A COMMENT