KIYAMA NI NINI?

Maswali ya Biblia No Comments

Neno kiama au kiyama lina maana ya “Siku ya ufufuo”

Neno hili kiyama linapatikana sehemu mbalimbali Katika Maaandiko, hivi ni baadhi ya vifungu

Mathayo 22:23-28

[23] Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza,

[24]wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao.

[25]Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake.

[26]Vivyo hivyo wa pili naye, na wa tatu, hata wote saba.

[27]Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye.

[28]Basi, katika kiyama, atakuwa mke wa yupi katika wale saba? Maana wote walikuwa naye.

Hayo Maaandiko yanazungumzia mafarisayo  walitaka kujua kutoka kwa Yesu siku ya ufufuo wa wafu, mambo ya ndoa yatakuwaje.?

Soma pia..Wafilipi 3:10-11

[10]ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake;

[11]ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu.

Akimaanisha afikie siku ya ufufuko wa wafu.

Neno hilo utalisoma pia katika vifungu hivi;

2 Timotheo 2:17-18,22

[17]na neno lao litaenea kama donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto,

[18]walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata kuipindua imani ya watu kadha wa kadha.

Pia na sisi wakristo hatuna budi kuyaelekeza mawazo yetu katika ufufuo wa wafu, Tumaini hilo ni lazima liwepo ndani yetu. Na ufufuo huo utakuja siku ile ya UNYAKUO ambapo parapanda italia, wafu wote waliokuwa makaburini waliompokea Kristo, watafufuliwa na moja kwa moja wataungana na sisi tuliohai kisha kwa pamoja tutapaa kumlaki Bwana Yesu mawinguni.

Swali la kujiuliza. Je, tumejipangaje kwa ajili ya siku hiyo ya kiyama? Je matendo yetu wanastahili kukubaliwa?

Majibu sote tunayo.

Tukumbuke kuwa Siku ya kiyama ipo karibuni sana.

Shalom

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *