KIMA NI NINI KIBIBLIA?

  Maswali ya Biblia

JIBU…

Tukianza na maana tunayoifahamu..Kima ambaye ni mnyama jamii ya nyani, ila biblia imeelezea kwa utofauti kidogo..

Na maana halisi ya Neno kima kwenye biblia ni ni thamani ya kitu Katika Pesa, kwa mfano mzuri tunaweza kusema kima cha mchele ni 2000 ,ni kusema thamani ya mchele ni 2000

Na tunalipata hapa…

Mithali 31:10
[10]Mke mwema, ni nani awezaye kumwona?
Maana kima chake chapita kima cha marijani.

Hapa anaelezea thamani ya mke mwema jinsi ilivyo, anasema inazidi thamani ya madini ghali ya marijan( Ruby)

Mathayo 27:9
[9]Ndipo likatimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema, Wakavitwaa vipande thelathini vya fedha, kima chake aliyetiwa kima, ambaye baadhi ya Waisraeli walimtia kima;

Mambo ya Walawi 27:11-14
[11]Na kama ni mnyama ye yote asiye safi, wa namna ambayo hawamsongezi kwa BWANA, basi atamweka huyo mnyama mbele ya kuhani;


[12]na kuhani atamtia kima, akiwa mwema akiwa mbaya; kama wewe kuhani utakavyomtia kima, ndivyo itakavyokuwa.


[13]Lakini kwamba ataka kumkomboa kweli, ndipo atakapoongeza sehemu ya tano juu ya hesabu yako.


[14]Na mtu atakapoiweka nyumba yake iwe wakfu kwa BWANA ndipo kuhani ataihesabu kima chake hiyo nyumba, ikiwa njema ikiwa mbaya; kama kuhani atakavyoihesabu kima chake ndivyo itakavyokuwa.

Pitia tena pia Walawi 27:23, Ayub 18:28, Matendo 7:16

Je, kipo kima kinachozidi thamani ya Bwana Yesu?

Tukimuangalia Yuda pamoja kote na kumuuza Bwana kwa kima cha fedha,na kupokea thamani kubwa ya pesa lakin mwisho wa siku aliona thamani ya Yesu hailinganishwi na chochote Katika ulimwengu huu,akachukua maamuzi ya kuzirudisha fedha zile na kuamua kujinyonga…

Ikiwa ndugu watu waovu wanauona uthamani wa Bwana Yesu Katika Maisha yao,vipi wewe unayeona kazi yako ni bora kuliko Mungu,anasa ni bora kuliko kwenda kanisani huoni umemuuza Mungu kwa kima cha fedha,

Uthamani wako umeuweka kwa nani, ni huu ulimwengu au kwa Bwana Yesu aliyekuumba na kukupa pumzi ya bure,(jibu unalo) biblia inasema itakufaidia nini kuupata ulimwengu mzima alafu ukapata hasara ya nafsi yako..

Tubu leo kwa kumaanisha kabisa kumrudia Mungu na thamani yako itakuwa kubwa..

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT