Fahamu maana ya Muhubiri 9:11 Si wenye mbio wote washindao katika Michezo.

  Maswali ya Biblia

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Ukiangalia watu wengi wanaofanikiwa katika ulimwengu huu mara nyingi sana husifiwa kwa juhudi, walizonazo pengine hata wao wanapotoa ratiba zao kwa siku zinakuwaje mara nyingi huwa tunaona ni juhudi zao, ustadi wao pengine Elimu zao nk kwa jicho la kawaida unaweza kusema ni kweli na kuna uhalisia ndani yake.

Lakini sasa tukirudi katika Neno hili alilolizungumza Sulemani kwa hekima aliyopewa na Mungu Kuna jambo la tofauti kidogo hebu tusome..

Mhubiri 9:11 “Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote”.

Ukisoma kwa makini hapo utaona Sulemani anaanza na kusema “Nikarudi na kuona chini ya jua…..” ikiwa na maana kuwa ni jambo ambalo amekuwa akiliona mara kwa mara rikijirudia rudia si jambo ambalo linatoke mara moja bali mara nyingi nyingi linatokea duniani. Hata sisi huenda tumewahi kuliona mahali fulani lakini tusijue ama kulitafakari. Lakini leo tutatazama ni kwa namna gani.

Sasa Si wote wenye Maarifa, ufahamu, Ustadi, mbio, Hekima nk, mara zote ndio zinazowasaidia kufanikiwa sana kuliko wale wasiokuwa na vitu hivyo. La!,

Ukisoma mwishoni anamalizia na kusema “Lakini wakati wa bahati huwapata wote” unaona hapo!, ikitufundisha pia kuwa majira siku zote habadilika wala hayakai hivyo hivyo milele.

Maana yake ni nini basi ni sawa na leo mtu anaweza akawa na vyeti vya Elimu ya juu sana kama Masters,PHD, nk ikamfanya awe na mafanikio makubwa sana katika maisha yake na nchi kwa ujumla, lakini kuna mwingine ambae hana Elimu kubwa hivyo lakini ana kipawa cha Hekima,ujuzi ama kipaji fulani ambao kazaliwa nao wala hajajifunza kokote kikamfanya apate milango ya mafanikio mingi na akafanikiwa zaidi ya yule mwenye Elimu kubwa.

Hii inatufundisha dhahiri kabisa kuwa Mungu ndie anaetoa na si Mwanadamu kwa utashi wake na nguvu zake.

Ukimsoma Yusufu mpaka anakuwa waziri mkuu wa Misri(dunia yote) si kwamba alikuwa na Elimu kubwa sana ya uchumi nk lakini ni Neema tu alipata maana hakustahili kabisa kwanza hakuwa mmsri na pili alikuwa na kesi ya ubakaji halafu anakuwa waziri Mkuu hebu tafakari kwa mwanadamu jambo hili linawezekana?? Lakini yote yako mikononi mwa Bwana. Haleluya!,

Mtume Paulo anasema..

Warumi 9:16 “Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu”.

Hivyo sisi hatujui pia wakati wetu ni upi!, lakini tendelee kuwa ni wanyeyekevu kwa Bwana yeye atatukweza kwa wakati wake wala tusiwe ni watu wenye kuwadharau wengine wala kuona sisi ndio wateule tumefika tusiwe hivyo kabisa kama wana wa Mungu wakati wako ukifika hata Bwana hataangalia una cheti ama huna umesoma ama hujasoma hivyo endelea kunyeyekea tu kama Neno linavyotwambia.

1Petro 5:6 “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake”;

MARANATHA.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT