NINI MAANA YA KUTEKEWA?

  Maswali ya Biblia

JIBU.. Tusome ili tupate kuelewa..

Mathayo 22:8-12
[8]Kisha akawaambia watumwa wake, Arusi i tayari, lakini wale walioalikwa hawakustahili.


[9]Basi enendeni hata njia panda za barabara, na wote mwaonao waiteni arusini.


[10]Watumwa wale wakatoka wakaenda njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu kwa wema; arusi ikajaa wageni.


[11]Lakini alipoingia yule mfalme ili kuwatazama wageni wake, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi.


[12]Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Naye akatekewa.

Maana halisi ya neno kutekewa,sio kutekewa kitu kama maji kama tunavyofahamu , Hapana, bali kutekewa lina maana ya KUKOSA MANENO..

Pale unapokosa majibu ya maswali fulani unayoulizwa hapo tunasema umetekewa majibu,ndo mana Katika habari hiyo Bwana Yesu anamuelezea mtu aliyetekewa baada ya kukutwa hana vazi la harusi..

 Na hii inatuonyesha pia hata Katika siku za mwisho Bwana Yesu atawakataa watu wengi na yote kwasababu hawana vazi la harusi, na tunajua vazi ni Matendo mema wa waaminio..

Ufunuo wa Yohana 19:8
[8]Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.

Katika siku hiyo wengi watadhani imani zao,au dini zao,zitawapa kibali cha kuingia Mbinguni lakini kumbe UTAKATIFU Ndio tiketi ya kumwona Mungu..

Waebrania 12:14
[14]Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;

Kwasababu utakatifu hatuupati kwa jitihada zetu wenyewe bali ni nguvu ya Mungu kwa Msaada wa Roho Mtakatifu..

Na kanuni ya kuishi maisha ya utakatifu ni KUTUBU na kubatizwa Katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo, na hapo unapokea Roho Mtakatifu atakayekusaidia kuishi Katika utakatifu..

Na hapo mbele za Bwana tunakuwa tumeonekana tumevaa vazi la harusi hivyo ile siku ya mwisho hatutatekewa mbele zake,hatutakosa maneno..

Lakini tukikosa hayo na kujitumainia Katika vitu vingine vya kidini, thiolojia, na tamaduni zetu wenyewe basi siku ile tutakosa chakujibu.. 

Mathayo 7:21-23
[21]Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.


[22]Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?


[23]Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

Maran atha

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT