Mtu Mwenye “Kitango” Ni Mtu Wa Namna Gani Kibiblia?

  Maswali ya Biblia

Kulingana na vifungu hivi biblia imetaja neno hili

Mithali 20:13 “Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo.

Mithali 20:19 “Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Basi, usishirikiane naye afunuaye midomo yake sana”.

Neno hili kitango linamaanisha Mtu “MMBEA”, mtu ambaye yuko tayari kusema  kila kitu anachosikia au kuona kutoka kwa wengine. Mtu wa aina hii mara nyingi huhusishwa na usambazaji wa siri ambazo si vyema kufichua.

Kwa mfano, mtu anaweza kukaribishwa ndani ya nyumba ya jirani na kugundua mapungufu ya nyumba, ambayo wamiliki hawakutaka kufichua kwa kusema kumbe hili lipo hivi au lipo vile. Mtu huyu anaweza kufichua siri hizi kwa wengine, bila kujali utu wao.

Mtu mwingine anaweza kuambiwa siri na rafiki yake, lakini akatoka na kuitangaza mtaa mzima hadi habari zimrudie. Mtu huyu ni hatari na hapaswi kuaminiwa. Biblia inaonya kwamba tusishirikiane na watu wanaoweza kufichua siri za wengine, kwa kuwa ni wazi kwamba tayari wameshafanya hivyo basi si vizuri kumshilikisha.

Jambo hili limekuwa chanzo kikuu cha watu kutokupiga hata hatua katika maisha ya kiroho na kimwili kwa sababu ya kukosa kuuzuia ndimi zao, ukitaka kufurahia maisha, ni muhimu kuudhibiti ulimi na kinywa chako usiwe kila kitu unachokiona au kukisikia lazima ukitangaze kwa wengine.

Na kwa kufanya hivyo, utafurahia maisha yako wenyewe pia utampendeza Mungu, ambaye hachukui mambo yetu ya siri kiholela.

Mathayo 5:48 “Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu”.

Jambo la kuzingatia Tusipende kusambaza siri za wengine tutake amani na kila mtu na upendo ndani yetu.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT