Kumbukumbu la Torati 10:17 Kwa maana BWANA, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea nyuso za watu, wala hakubali rushwa.
JIBU: Kibiblia ukikutana na neno mungu/miungu limeandikwa kwa herufi ndogo,(isipokuwa tu pale ambapo ni mwanzoni mwa sentensi, kwasababu kisarufi sentensi yoyote ikiianza ni lazima ianze na herufi kubwa), basi ujue anayezungumziwa hapo sio yule Mungu muumba wa mbingu na nchi (Yehova), bali linawakilisha miungu ya aina mbili;
Aina ya kwanza ni sanamu: Ambazo watu wanaziabudu, au mashetani.
Aina ya pili: Ni watakatifu.
Sasa Mungu anaposema yeye ni Mungu wa miungu, hamaanishi hiyo aina ya kwanza ya miungu, bali hiyo ya pili yaani watakatifu.
Sisi tuliozaliwa mara ya pili, mbele za Mungu ni miungu. Tunalithibitisha hilo katika maneno ya Bwana Yesu mwenyewe;
Yohana 10:33 Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu.
34 Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu?
35 Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka);
36 je! Yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?
Na ndio maana katika vifungu kama hivi, utatambua miungu wanaozungumziwa hapo sio masanamu bali watakatifu tusome;
Zaburi 97:7 Na waaibishwe wote waabuduo sanamu, Wajivunao kwa vitu visivyofaa;
Enyi miungu yote, msujuduni Yeye.
Zaburi 136:2 Mshukuruni Mungu wa miungu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Lakini swali la msingi la kujiuliza, wewe kama mwanadamu, je mbele za Mungu ni nani?
Kumbuka watakaomwona Mungu, ni lazima na wao pia wawe kama Mungu. Ikiwa wewe maisha yako ni kama ya shetani, basi jiandae ukifa kwenda kukutana na baba yako shetani.
Ikiwa hujazaliwa kwa maji na kwa Roho sawasawa na maneno ya Bwana Yesu (Yohana 3:5), ni uthibitisho tosha kuwa wewe ni wa kuzimu. Haijalishi una dini Au dhehebu zuri kiasi gani.
Tubu ndugu ikiwa bado upo nje ya Kristo, muda tuliobakiwa nao ni mchache, Parapanda inakwenda kulia hivi karibu, karamu ya mwanakondoo ipo mlangoni. Kuangamizwa kwa dunia na waovu kumeshafika.
Ikiwa utasema siku ya leo sitaki inipite, bila kuyasalimisha maisha yangu kwa Kristo, basi fungua hapa kwa ajili ya mwongozo wa sala ya Toba. >> https://wingulamashahidi.org/2020/07/22/kuongozwa-sala-ya-toba/
Mungu akubariki sana.
MADA ZINGINEZO:
JIANGALIENI BASI JINSI MSIKIAVYO.
Je! Yohana mbatizaji alibatizwa na nani?