MGANDA NI NINI?

Maswali ya Biblia No Comments

Jina la Bwana libarikiwe.
Karibu tujifunze neno la Mungu

Neno mganda utakutana nalo sehemu kadha wa kadha katika biblia.

Tusome..
Walawi 23:10
Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapokuwa mmekwisha ingia hiyo nchi niwapayo, na kuyavuna mavuno yake, ndipo mtakapomletea kuhani mganda wa malimbuko ya mavuno yenu;

[11] naye atautikisa mganda mbele za Bwana ili kwamba ukubaliwe kwa ajili yenu; siku ya pili baada ya Sabato kuhani atautikisa.

[12] Na siku hiyo mtakayoutikisa mganda, mtamsongeza mwana-kondoo wa kiume mkamilifu wa mwaka wa kwanza awe sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana.

Pia soma Mwanzo 37:6

Mganda ni matita ya mazao yoyote yaliyovunwa na kufungwa pamoja, mfano ngano ikivunwa shambani, hufungwa kwanza matita matita baadaye zinakusanywa zote pamoja, ndipo huenda kukobolewa na kusagwa, sasa hayo matita matita ndio huitwa miganda.

Tusome..
Kumbukumbu 24:19 Uvunapo mavuno yako katika shamba lako, ukasahau mganda shambani, usirudi kuuchukua; na uwe wa mgeni, au yatima, au mjane; ili Bwana, Mungu wako, akubariki katika kazi yote ya mikono yako.

Hakimaanisha ikitokea, umeenda shambani kuvuna, ukakusanya miganda kumi au zaidi, sasa wakati unaondoka ukasahau mmoja, walikatazwa kurudi nyuma kuuchukua, bali wauache kwaajili ya mayatima na wageni, Kwa sababu masikini waliruhusiwa kuingia kwenye mashamba na kuokota vile vilivyosalia.

Inatufundisha nini hapo?

Kuna wakati Mungu ataruhusu usichukue kila kitu ulichonacho/ usikusanye miganda yote uliyonayo, ili, mayatima, mgeni, na wajane nao wafaidike. hivyo ukiona umesahau kimoja katika vingi ulivyonavyo (mfano nguo nk )usiwe mwepesi wa kukirudia ili kukichukua, utajiepusha na baraka zako, maana hujui kwanini Mungu amekusaulisha.

Hivyo na sisi tusiwe na tabia ya kubeba miganda yote.

Bwana akubariki.

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Washirikishe na wengine habari hizi njema Kwa kushea.. Au wasiliana nasi kwa namba hii, 255789001312,255693036618

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *