Nini maana ya kura hutupwa katika mikunjo ya nguo,

Maswali ya Biblia No Comments

Mithali 16:33
[33]Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo;
Lakini hukumu zake zote ni za BWANA.

JIBU..

Kipindi cha zamani kura zilipigwa kwa namna nyingi nyingi, na njia iliyoonekana rahisi na nyepesi ni hiyo, ambayo ni Kipande kidogo cha mfano wa shuka,kilitumiwa kukusanya kura walizopiga watu ambazo waliaziandika kwenye vibao vidogo vidogo au mawe na kisha huchanganywa,kukoroga na kile kitakachokuwa cha kwanza kuchukuliwa huko huwa ndo sahihi…

Na aina nyingi zilitumika kuleta majibu sahihi Katika upigaji wa kura…

Upo wakati ambao pia Mungu aliruhusu baadhi ya vitu viamuliwe kwa kupiga kura, mfano kugawanya nchi, pitia Hesabu 26:55, Yoshua 18:6-10) ijapokuwa si kila jambo alitumia njia hii, wakati mwingine alisema kwa kupitia manabii, kupitia maono,ndoto..

Sasa anamaanisha nini, anaposema Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo; Lakini hukumu zake zote ni za BWANA.?

Ikimaanisha ingawaje tendo la kupiga kura linaonekana ni la kibinadamu, lakini likifanyika Katika Bwana basi majibu ya Kweli hutoka kwake, fahamu huyo atakayechaguliwa au kitu kupendekezwa jua jibu hilo ni kutoka kwa Bwana..

Katika Maaandiko tunamwona Mtume Mathiya akichaguliwa kwa kupiga kura, lakini tunaona kabla ya kupiga kura walimtanguliza Mungu kwanza,walimuomba Mungu aingilie kati uchaguzi wao,na kisha kila mmoja akaandika pendekezo lake, na jawabu likatoka ni Mathiya,likawa jibu sahihi kutoka kwa Mungu..

Matendo ya Mitume 1:23-26
[23]Wakaweka wawili, Yusufu, aitwaye Barsaba, aliyekuwa na jina la pili Yusto, na Mathiya.


[24]Kisha wakaomba, wakasema, Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili,


[25]ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe.


[26]Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja.

Tunaweza kukatoa malaumu mengi kwa viongozi tuliowachagua,tukajua walituibia kura, kumbe sivyo” kwasababu kama Mungu asingetaka wawepo kwenye hizo nafasi basi wasingekuwepo tu,kwa kuwa yeye mwenyewe ndiye mwenye uwezo wa kuwamilikisha watawala iwe  ni waovu au watenda wema,hilo ni jukumu la Mungu mwenyewe…

Danieli 2:21[21]Yeye hubadili majira na nyakati; huuzulu wafalme na kuwamilikisha wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa;

Yapo mambo tutaona ni sisi wenyewe tumeayachagua au kuyataka yatoke,au yametokea kwa bahati, lakini kumbe ni Mungu alishayapanga kwasababu kwake havitokei kwa bahati bali viko kwa makusudi yake,yeye pekee ndiye mwenye uwezo wa kuyaruhusu yote na yakafanyika..

Sifa na utukufu vina yeye milele,Amina

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *