NINI MAANA YA UGONJWA WA KUFISHA?

Maswali ya Biblia No Comments

Yeremia 17:9
[9]Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?

Neno kufisha ni kitendo cha kusababisha kitu kiweze kufa, au kupoteza uhai wake..

Na hapo Maaandiko yanaposema moyo una ugonjwa wa kufisha, ina maana kuwa una ugonjwa wa kupelekea mauti, ni ugonjwa usiponyeka.. hi ikionyesha moyo una udanganyifu mbaya sana, moyo unaweza kukupeleka Katika mauti ya Mwilini mpaka rohoni..ndo mana tunamwona shetani akiwa kule Mbinguni hakudanganywa na mtu bali moyo wake ulimdanganya kwamba anaweza kuwa kama Mungu..

Na tunajua kilichotea,akatupwa chini na malaika zake waliofata udanganyifu wake,ni Jambo ambalo analijutia sana kwa hasara aliyoipata, Kwasababu udanganyifu hautoki kwa shetani,unaanza ndani yetu na tukiuchochea ndipo shetani anapata nafasi ya kuuzidisha zaidi..

Mithali 14:12
[12]Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu,
Lakini mwisho wake ni njia za mauti.

Utajiaminisha Katika uvaaji mbovu,kuvaa nguo fupi,vimini, suruali ukaona ni sawa kwasababu moyo wako unakuambia hivyo, kumbe unajiangamiza mwenyewe, unaweza kuabudu sanamu,na miti ndio njia ya kumwabudu Mungu kumbe unajimaliza kabisa..

Yesu Kristo ndio njia ya uzima na kweli, hakuna njia nyingine..ukilijua hilo utamsikiliza Mungu anasema nini kwenye neno lake na sio moyo wako unataka nini..

Bwana atusaidie sana..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *