WANYAPARA NI WATU GANI?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom, karibu tujifunze..

JIBU, Tusome..

Kutoka 5:14-16[14]Na wanyapara wa wana wa Israeli, ambao wasimamizi wa Farao wamewaweka juu yao, wakapigwa, wakiambiwa, Kwa nini hamkutimiza kazi yenu jana na leo; kwa kufanya matofali kama hapo kwanza?

[15]Basi wanyapara wa wana wa Israeli wakaenda, wakamlilia Farao, wakisema, Mbona umetutendea hivi, sisi watumwa wako?

[16]Watumwa wako hawapewi majani, nao wanatuambia, Fanyeni matofali; na tazama, watumwa wako wapigwa; lakini kosa hilo ni la watu wako mwenyewe.


Wanyapara ni watu waliopewa mamlaka ya kuwasimamia watumwa au wafungwa…

Ndani ya gereza kuna wafungwa ambao huteuliwa kuwa viongozi kwa wafungwa wenzao, viongozi hao ndio wanajulikana kama wanyapara…Kazi ya nyapara ni kupokea maagizo kutoka kwa askari mkuu wa gereza na kuyapeleka kwa wafungwa wenzake kisha kusimamia utekelezaji wa maagizo hayo japokuwa na yeye mwenyewe ni mfungwa…


Wakati wana wa Israel wapo utumwani huko Misri, askari wa Farao waliteua baadhi ya wafungwa kuwa wanyapara ili kuwasimamia wafungwa wenzake.. Askari walitoa maelekezo juu ya kazi fulani kisha wanyapara waliwaongoza wafungwa wenzao katika utekelezaji na ikiwa watumwa hawatafanya kazi inavyotakiwa basi wanyapara ndio walikuwa wa kwanza kuwajibishwa maana wale askari wa Farao waliwaangalia kwanza wanyapara kabla ya watumwa…

Kutoka 5:14 “Na wanyapara wa wana wa Israeli, ambao wasimamizi wa Farao wamewaweka juu yao, wakapigwa, wakiambiwa, Kwa nini hamkutimiza kazi yenu jana na leo; kwa kufanya matofali kama hapo kwanza?

Hivi leo shetani ameweka wanyapara juu ya watu wote anaowatumikisha katika dhambi. Maandiko yanasema kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi, na ikiwa ni mtumwa basi atakuwa na nyampara wake.


Ikiwa mtu anaishi katika uzinzi au uasherati yule anaishi naye kama mume au mke ni nyapara wa shetani kwako ndo maana dhambi hiyo inakutesa kwa sababu wote mnaishi ndani ya dhambi, hata kwa dhambi nyingne ni hivyo hivyo shetani atakuwekea tu mnyapara…

Nafasi bado unayo ya kukataa kuwa katika utumwa wa shetani na kuwa nyapara wake, mgeukie Yesu uwe chini ya mwongozo wa Roho mtakatifu ukatende mema upate uzima wa milele…


Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *