BIBLIA TAKATIFU NI NINI?

Je! Biblia ni nini?

Biblia ni neno lililotoholewa katika lugha ya kigiriki lenye maana ya “mkusanyiko wa vitabu vitakatifu”. Na pale kinapokuwa kimoja huitwa ‘Biblioni’

Na katika biblia hii ambayo ni vitabu vitakatifu ina jumla ya  mkusanyiko wa vitabu 66 na ndani ya vitabu hivi vimegawanyika makundi mawili ambayo ni Agano la kale na Agano jipya, katika agano la kale kuna vitabu 39, na  agano jipya 27 mkusanyiko huu ndiyo  unaleta jumla ya  vitabu 66 vitakatifu vyenye maneno ya Mungu.

Na vitabu hivi viliandikiwa na wanadamu  kabisa  kwa uvuvio wa Roho mtakatifu, maana Mungu siku zote hufanya kazi ndani ya wanadamu

Sawa sawa na andiko la 

Warumi 8:28

[28]Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. 

Na Mungu aliwatumia watu hawa hili waweze kuandika habari zihusuzo, Sheria ya Mungu, maneno ya Mungu, Uweza wa Mungu, Ukuu wa Mungu, Upendo wa Mungu na Utukufu wa Mungu, haya yote Mungu aliyaruhusu yaandikwe hili wanadamu wamtambue Mungu katika ukamilifu wote.

Na watu aliowatumia walikuwa makundi tofauti tofauti katika kuwasilisha meneno matakatifu, alitumia manabii, wafalme,  watoza ushuru, wavuvi nk.. 

Hiyo yote kuonyesha kuwa Mungu anao uweza wa kumtumia yoyote kuwasilisha kusudi lake 

Nini kusudi kuu la biblia (vitabu vitakatifu )

Mungu aliruhusu vitabu hivi viwepo hili kumfunua Yesu Kristo, yaani biblia nzima kiini kikuu ni Yesu Kristo, hivyo katika unabii wote, habari zote ndani ya biblia zinamfunua Yesu Kristo usomapo biblia iwe katika angano la kale au jipya muone Kristo tu

Na biblia ndiyo kitabu cha thamani na cha pekee katika maisha, ukikosa kujua maneno ya Mungu haya basi jua kabisa utapelekwa pelekwa  na kuyumbishwa na dunia hii lakini neno la Mungu likikaa kwa wingi ndani yako kwa kujifunza, kutafakari, na  kufundishwa  itakufanya uimalike bila kuchukuliwa na mafundisho ya uongo 

Wewe kama mtu uliyekombolewa na Yesu Kristo penda kusoma biblia kila wakati kila saa na siku zote, usisubiri jumapili hadi jumapili ndipo ufungue biblia yako, acha huo utoto amka sasa anza kutaka Hekima na Maarifa yatokayo mbinguni kupitia Neno la Mungu

1 Yohana 2:5

[5]Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake.

Ubarikiwe

Je! Umemwamini Yesu Kama Bwana na mwokozi wa maisha yako? Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo, basi fungua hapa kwa mwongozo wa kumkaribisha Yesu maishani mwako >>> http://Kuongozwa sala ya toba

Kwa mafundisho mengine mengi kwa kina jiunge na channel yetu ya mafundisho whatsapp kwa kubofya hapa >>

Pia ukihitaji kuokoka, ushauri, maombi, au majibu ya maswali ya kibiblia. Tuandikie kwa namba zetu hizi +255789001312/ +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine

Kuzumbua Ni nini kama inavyotumika kwenye biblia.(Walawi 6:3)

SABURI NI NINI KATIKA BIBLIA?

Arabuni maana yake ni nini? ( Waefeso 1:14)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *