NINI MAANA YA UPOLE? 

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

Nakukaribisha tujifunze Maneno ya Uzima ya Bwana Yesu…

Upole ni ile hali ya kutokuonyesha uharibifu kwa mtu au kwa viumbe, na upole umeenda mbele Zaidi pale ambapo unakuwa na uwezo wa kuonyesha madhara fulani kwa mtu lakini hutumii nafasi hiyo kumdhuru..

Mfano mzuri tumtofautishe nyoka na Ngamia..

Nyoka ni kiumbe chenye udhaifu kisichokuwa na uwezo wa kutembea wala kushika tofauti na mnyama ngamia mwenye Nguvu na uzito, 

Kwanini kwako itakuwa rahisi kumkimbilia Ngamia wala si nyoka?

Ni kwasababu Ngamia ni mpole na hana wepesi wa kutumia nguvu zake kukudhuru, tofauti na nyoka ukimsogelea tu anakuletea madhara makubwa…

Ndivyo pia katika wanadamu,wapo wapole lakini pia wapo wasio wapole..

Katika Maaandiko wapo watu wawili waliomifano na kushuhudiwa kuwa ni wapole..Wa kwanza ni Bwana Yesu, Wapili Musa..

  1. YESU KRISTO

 Biblia inasema..

Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, *nami nitawapumzisha. 29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

Yeye alikuwa mpole kama mwanakondoo mpaka Roho Mtakatifu kupelekea kushuka juua yake mithili ya njiwa..Na kawaida ya njiwa hatui juu ya sehemu isiyokuwa na utulivu,wala kutua juu ya mnyama mkali…

Na ndo mana Mungu alimtukuza sana Bwana Yesu, leo hii watu wote wanamkimbilia Kristo kwasababu ni Mpole rohoni,Kumbuka pia Bwana Yesu anajulikana kama simba wa Yuda”na tunajua tabia za simba sio upole, lakini kuja kwa Bwana ni Katika upole…

2) MUSA

Na Mwingine Katika biblia ni Musa,na tujiulize ni kitu gani alichokuwa nacho Musa kikamfanya awe Karibu na Mungu namna ile?

Sababu ni Upole wake,

Biblia inasema..

 Hesabu 12:3 “Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi”. 

Kuzidi kwa upole Ndiko kulimfanya Musa kuwa karibu sana na Mungu kuliko wanadamu wote duniani…

Na sisi tukitaka kumkaribia Mungu kanuni ni hiyo hiyo, hatuna budi kuwa wapole.

Na njia za kuwa wapole ni pamoja na ;

 KWA KUJISHUSHA 

Unapojionyesha kukubali kuonekana wewe ni dhaifu,ni hatua ya kuw mpole, lakini ukitaka kujiona wewe ni shujaa wa mambo yote na kukataa kuchungwa,utabaki kuwa mbuzi na si mwanakondoo..

 KWA KUZIZUIA HASIRA ZETU

Tunakuwa watu wa kujitahidi kuvizuia sana vinywa vyetu, na hasira ndio mwanzo wa ugomvi na vita,ukiweza kudhibiti hasira zako hata kama utaudhiwa kiasi gani,hujibu, basi ndio mwanzo wa kujenga upole ndani yako..

 KWA KUSOMA NENO NA KUOMBA

Hii ni mojawapo ya tiba kubwa sana,kama vile ukitaka kuelewa hesabu soma hisabati, ndivyo ilivyo ukitaka kuwa na upole usiikwepe biblia, Kwasababu hiyo ndio itakupa misingi ya kuwa mpole kama Kristo,vile vile kusali kunaukaribisha uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yako na kufikia kiwango hicho.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.

Piga namba hizi: *+255693036618 au +255789001312*

Masomo mengine:

UNADHANI WAKATI WAKO SAHIHI WA KUMTII MUNGU BADO?

IKAWA, MFALME ALIPOYASIKIA MANENO YA TORATI, ALIYARARUA MAVAZI YAKE.

KWA MAANA ISRAELI AMETENDA KWA UKAIDI, KAMA NDAMA MKAIDI;

Mtume Paulo alikuwa na maana gani kusema “Kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia” Je! Alikuwa akijigamba?(Wafilipi 3:6)

LEAVE A COMMENT