Nakusalimu katika jina la Bwana wetu na Mwokozi wetu Yesu Kristo!
JIBU:
IJUMAA KUU. Hii ni siku maalumu inayokumbukwa na wakristo wengi duniani. Ni siku ya ijumaa kabla ya jumapili ya pasaka ambapo wakristo wengi duniani wanaiadhimisha kifo cha Mwokozi wetu Yesu Kristo. Siku hii huadhimishwa kila mwaka na Wakristo wengi Duniani.
Kwanini iitwe ijumaaa kuu??
Na isiitwe ijumaa ya shida na taabu ya Mwokozi wetu pale Kalvari? Maana pia ilikuwa ni siku ya furaha kwa falme za giza kufurahia Mwokozi wa ulimwengu anakufa Kalvari?.
Kwa namna ya kawaida ama kwa jinsi ya kibinadamu ni siku ambayo si nzuri wala haifurahishi, lakini , katika ulimwengu wa Roho ni siku ambayo ni kuu sana na ya furaha sana tena sana kwetu sisi wanadamu. Ambayo hata manabii walitamani kuiona hii siku lakini hawakuweza kabisa.
Kwani ni siku pekee ambayo sisi wanadamu kwa mara ya kwanza tunafutiwa hati ya mashtaka yetu ya hukumu ambayo tulikuwa nayo Tangu tulipoanguka pale Edeni.
Kama Kristo Yesu Mwamba wa uzima ,Bwana wa Mabwana asingelitufia pale msalabani, Tusingelipata ondoleo la dhambi yaani (Msamaha wa Dhambi.) Hivyo huu kwetu ni ukombozi mkuu sana.
Ni siku ambayo inapofika na kuiadhimisha sio siku tena ya huzuni kwetu na kilio bali ni siku ya furaha na kumsifu Mwokozi wetu kwa kile alichokifanya kwa ajili yetu. Maana katika siku kama hiyo tulipata ukombozi yaani tuliwekwa Huru mbali na dhambi zetu na kufanywa kuwa wana wa Mungu pamoja na Kristo Yesu. “HALELUYA” asifiwe Mwokozi. Hivyo ni sahihi kuitwa ijumaa kuu na sio ijumaa ya taabu, shida,vilio na simanzi bali ni sahiji kabisa kuitwa IJUMAA KUU.
Kama Kristo asingekufa leo hii tusingelipata msamaha wa dhambi.
Waebrania 9:12″ Yeye aliingia Mahali Patakatifu mara moja tu, akiwa amechukua, sio damu ya mbuzi na ng’ombe, bali amechukua damu yake yeye mwenyewe, akatupatia ukombozi wa milele”
Je Kuna agizo lolote la kutokula nyama siku ya ijumaa kuu?.
Jibu ni la!, kutokula nyama ni maagizo ama mapokeo tu ya kanisa la Romani katoliki. Wala hakuna sehemu yoyote biblia imesema siku ya ijumaa kuu hakuna kula nyama.
Lakini ni utaratibu waliojiwekea wao tu kwa madai ya kumheshimu Kristo kwa kuutoa mwili wake sadaka kwa ajili yetu sisi. Maana nyama ni chakula cha starehe( furaha). Wameweka utaratibu kama huo ili kuyatafakari mateso ya Mwokozi wetu Kristo Yesu pale Kalvari. Na agizo hili(pokeo) katika kipindi chote cha siku 40 za mfungo kila ijumaa hawali nyama lakini pia katika siku ya kupaka majivu.
Sasa hakuna maandiko yanayosema usile na ukila ni kosa, si dhambi ukifanya hivyo kula ama kutokula si kosa ni maamuzi ya mtu .
JE! KUIADHIMISHA SIKUKUU HII NI DHAMBI?
HAPANA si dhambi, biblia haijatoa kazo ama agizo la mtu yeyote kuiadhimisha siku fulani anayoona yeye kwa ajili ya Mungu wake. Ni kwa namna yeye anavyoona ama kuamini moyoni mwake. Hebu turidhibitishe hili katika maandiko.
Warumi 14:5 “Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe.
6 Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu”.
Ikiwa kwako utaona siku ya ijumaa ni siku ya kawaida tu kwako si kosa wala si dhambi , pia usimhukumu pia anaeiadhimisha hiyo siku kwake kuwa ni kuu na takatifu usimhukumu kwa hilo maana anafanya hivyo kwa Mungu wake.
Na zaidi sana siku zote njema wala hakuna siku mbaya, siku zote ni za Mungu wala si za Shetani. Lakini pia ukiona mfungo huo wa siku arobaini (40) hauna maana kwako pia ni sawa wala si dhambi na hautahukumiwa katika hilo. Wala anaefunga na kuona mfungo huo kwake ni mzuri kwa ajili ya kumkaribia Mungu pia ni sawa na hafanyi dhambi na pia vile vile asikuhukumu katika hilo.
Je umeokoka? Umemuamini Yesu Kristo? Kama bado hujachelewa mlango uko wazi Kristo Yesu anakupenda. Mwamini na ubatizwe katika maji mengi na kwa Jina la Yesu Kristo upokee ujazo wa Roho Mtakatifu ufanyike kuwa mwana wa Mungu (Yohana 1:12)
Ubarikiwe sana.
Washirikishe na wengine ujumbe huu.
Kwa mawasiriano zaidi +255693036618/+255789001312
Jiunge pia na Channel yetu ya WhatsApp.
“ NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Masomo mengine:
UFALME WA MUNGU NI NINI, ULITOKA WAPI NA ULIANZA LINI? (Sehemu ya 02)