Pasaka ni nini? Na Je! ni sawa kuiadhimisha?

Jina la Bwana na mwokozi wetu, Yesu kristo litukuzwe.

Karibu tujifunze maneno ya Mungu wetu, ambayo ndio taa ya miguu yetu  na mwanga wa njia zetu. 

Je! Pasaka ni nini? 

Kabla ya kuangalia pasaka ni nini, tuangalie asili ya ili neno Pasaka. 

Asili ya neno Pasaka, tunaliona pale Mungu alipokuwaa akiongea na Musa pamoja  na Haruni, (Kutoka 12:1) kuhusu kuondoka kwa wana wa Israeli kutoka kwenye nchi ya utumwa Misri kuelekea kwenye nchi ya ahadi kanaani.

Mungu aliwapa maagizo ya kumchinja mwana kondoo mmoja katika kila nyumba ya  wana waisraeli na kuichukua damu ya mwana kondoo huyo na kuipaka kwenye vizingiti na miimo ya nyumba zao ili mapigo  ya Mungu aliyokuwa ameyakusudia juu ya wazaliwa wa kwanza wote wa msiri juu ya mwanadamu na wanyama itakapopita isiwape na wao. 

Hapo ndipo Mungu alipowaambia mtamla huyo mwanakondooo ni Pasaka ya Bwana.

Tusome..

Kutoka 12:11 Tena mtamla hivi, mtakuwa mmefungwa viungo vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; NI PASAKA YA BWANA

12.Maana nitapita kati ya nchi ya misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana. 

13. Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu NITAPITA JUU yenu, lisiwapate pigo lolote likawaharibu, nitakapoipiga  nchi ya Misri. 

14. Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa Bwana; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote, Kwa amri ya milele.

Hivyo kile kitendo cha kupita kwa yule malaika wa mapigo juu ya damu ya yule mwanakondoo, iyo ndiyo  pasaka. maana tafsi ya neno Pasaka kwa kiswahili ni   PITA JUU, kwa kigiriki “pascha” na kwa kiingereza, passover, hivyo tunaweza kusema pasaka kwa kiswahili  tafsifi yake ni PITA JUU au VUKA  UPITE. 

Lakini katika agano jipya damu ya yule mwanakondoo inafananishwa na damu ya Bwana wetu Yesu kristo.

Kupitia damu yake, Yesu kristo, Bwana wetu, tunasafishwa dhambi zetu,  tunatoka misri (ulimwenguni) kuelekea kanaani yetu ( mbinguni) kwenye nchi ya ahadi. 

1 Wakorinto 5:7

Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. kwa maana PASAKA wetu amekwisha kutolewa sadaka, yaani KRISTO. 

Lakini wale wote walioacha kupaka damu ya mwanakondoo kwenye vizingiti na kwenye  miimo ya milango yao, walishiriki  mapigo ya wamisri, lakini wote waliotii waliokolewa kwa ile damu.

Je!  umesafishwa dhambi zako kwa damu yake, Mwokozi wetu Yesu kristo? 

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine ujumbe huu.

Kwa mawasiriano zaidi +255693036618/+255789001312

Jiunge pia na Channel yetu ya  WhatsApp. 

“ NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Masomo mengine:

Nini maana ya mstari huu? “Na amani ya Kristo iamue miyoni mwenu” (Wakolosai 3:15)

IKAWA, MFALME ALIPOYASIKIA MANENO YA TORATI, ALIYARARUA MAVAZI YAKE.

Kwanini Gombo la chuo lililokunjuliwa mbele ya nabii Ezekiel likikuwa limejaa maombolezo, na vilio na Ole ndani yake? (Ezekieli 2:10).

Je! Vazi takatifu kwa Mkristo ni kanzu kulingana na (Luka 9:3)?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *