Nini maana ya kwaresma. Je! ni sharti kuitimiza?

Kwaresma, linalotokana na neno la Kilatini Quadragesima, maana yake ni “Arobaini” na ni kipindi cha siku 40 cha kufunga kinachofanywa na baadhi ya wakristo kabla ya sikukuu ya Pasaka. Kusudi la mfungo ni kuwatayarisha Wakristo katika sala, toba, na unyenyekevu kwa  ajili ya Pasaka iliyopo mbeleni.

Kwaresma pia inahusishwa na Bwana kufunga kwa siku 40 akiwa jangwani, akijaribiwa na Ibilisi. Ikiwa na maana kuwa  wana wajibu wa kufunga siku 40 kama Bwana alivyofunga.

Hakuna sharti katika maandiko kutimiza Kwaresma, kwani haya ni mapokeo ambayo hayapingani na Neno la Mungu. Mapokeo mazuri hayapingani na Neno la Mungu, huku yale mabaya yanawafanya watu wawe wa kidini zaidi kuliko wa kiroho.

Kushika Kwaresma si dhambi, kwani ni wajibu wa kila Mkristo “kufunga na kuomba.” Kufunga ni lazima kwa kila mwamini, , iwe ni wiki moja, wiki mbili, siku 30, siku 40 au siku 50. Halikadhalika Tendo lolote la kufunga lisichukuliwe kuwa la kidini, kwani linaweza kuwa na matokeo madogo au liwe bure kabisa.

Kwaresma si wakati wa kujihusisha na mambo ya kidunia bali ni kuwa na amani ya akili na kuitesa nafsi. Ni wakati wa kutubu kweli kweli na kuomba kwa bidii, kuongeza juhudi katika mambo ya kiroho zaidi sawasawa na Isaya 58, inayotuongoza njia sahihi ya kufunga.. Ikiwa Kwaresima haifanywi kidini, ina matokeo makubwa kwa mhusika.

Mathayo 5:20 “Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni”

Kufunga ni nadhiri, kwamba unafunga siku 40, lakini ukisema unafunga halafu ndani ya mfungo huo unakuwa sio mwaminifu,  unaufanya mfungo wako usiwe na matokeo mazuri, Kama umeamua kufunga kwa kipindi Fulani ni vema umalize siku zote…

 Si lazima kufunga wakati wa Kwaresima, lakini ni wajibu kwa kila Mkristo. Ikiwa hutafunga wakati wa Kwaresima, tafuta wakati mwingine ufunge, na vi vema ikawa mara kwa mara.

Bwana akubariki

Ubarikiwe sana.

Shea na wengine ujumbe huu.

Kwa mawasiriano zaidi +255693036618/+255789001312

Jiunge pia na Channel yetu ya  WhatsApp. 

“ NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Masomo mengine:

JE! KUNA SIRI GANI KWENYE NAMBA AROBAINI (40) KATIKA BIBLIA?

Nini maana ya mstari huu “na mtu mmoja ajengapo ukuta, tazama, waupaka chokaa isiyokorongwa vema” (Ezekieli 13:10)

MADHARA YA KULISIKIA NENO LA MUNGU NA KUTOWAZA  KUCHUKUA UAMUZI WO WOTE ULE WA KULIFANYIA KAZI (KULITII)

TABIA NYINGINE YA IBILISI UNAYOPASWA KUIFAHAMU.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *