JE! KUNA SIRI GANI KWENYE NAMBA AROBAINI (40) KATIKA BIBLIA?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

SWALI: Bwana Yesu apewe sifa, naomba msaada wa jibu la swali hili, kwanini Nuhu alitengeneza safina kwa muda wa miaka arobaini (40), mvua ya gharika ilinyesha siku arobaini, WaIsraeli walikaa utumwani kwa miaka arobaini, na hata siku za mwizi pia ni arobaini, kumsahau marehemu ni baada ya siku arobaini, mtoto hunyolewa nywele baada ya siku arobaini, Yesu alifunga bila kula kwa siku arobaini, na hata wana wa Israeli walikaa jangwani kwa muda wa miaka arobaini, sasa je! Kuna siri gani kwenye namba 40?


JIBU: Kwanza kabisa, si kweli kwamba Nuhu alitengeneza safina kwa muda wa miaka 40 (maandiko hayajasema Nuhu alitengeneza safina kwa muda wa miaka arobaini). Na pia, biblia haijasema kuwa wana wa Israeli walikaa utumwani Misri kwa muda wa miaka arobaini, huo ni uongo,  Mungu alimwambia Ibrahimu kuwa, uzao wake utakuwa katika nchi isiyo yake na kuwatumikia watu wa nchi hiyo kwa Muda wa miaka mia nne (400).

Mwanzo 15:13 BWANA AKAMWAMBIA ABRAMU, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, WATAWATUMIKIA WATU WALENAO WATATESWA MUDA WA MIAKA MIA NNE.

14 Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi. 

Soma tena.

Matendo Ya Mitume 7:6 Mungu akanena hivi, ya kwamba wazao wake watakuwa wageni katika nchi ya watu wengine, NAO WATAWAFANYA KUWA WATUMWA WAONA KUWATENDA MABAYA KWA MUDA WA MIAKA MIA NNE.

7 Na lile taifa watakaowafanya watumwa nitawahukumu mimi, alisema Mungu; na baada ya hayo watatoka, nao wataniabudu mahali hapa. 

Na pia msemo huo wa siku za mwizi ni arobaini, hauna maana kwamba, huyo mwizi siku zake ni 40, hapana! Inawezekana mtu ikawa ni mara yake ya kwanza kuingiwa na tamaa kwenda kuiba, na kisha akapatwa na madhara; Mfano Akani mwana wa Karmi wa kabila la Yuda (Soma kitabu cha Yoshua sura 7). Au Inawezekana mtu maisha yake yote akawa anafanya kazi ya wizi na akafa kifo cha kawaida tu, ama kwa Malaria au presha. Vivyo hivyo pia suala la kumsahau au kumuomboleza kwa ajili ya marehemu, sio lazima ziwe siku arobaini, Wana wa Israeli waliomboleza siku 30 baada ya Musa kufa. 

Kumbukumbu 34:8 Wana wa Israeli wakamwombolezea Musa katika uwanda wa Moabu SIKU THELATHINI; basi siku za maombolezo ya matanga ya Musa zikaisha. 

Hivyo, kuomboleza baada ya kufiwa sio lazima ziwe siku Arobaini, ni uamuzi wa mtu, kwani wapo ambao hawafanyi kabisa hicho kitu. Mtu akifa na habari yake imekwisha (kinachofuata ni hukumu).


Lakini kuna umuhimu pia wa kufahamu Kwanini Wana wa Israeli walijaribiwa jangwani kwa muda wa miaka arobaini (Nehemia 9:21), au kwanini Kristo alijaribiwa nyikani kwa muda wa siku arobaini (Luka 4:1-2), au kwanini musa baada ya kukimbia misri alitimiza miaka arobaini kwa kuchunga kondoo jangwani kisha kurudi kuchunga taifa la Mungu.


Jibu ni kwamba, hiyo inawakirisha mwisho wa kumaliza Jaribu. Hata na sisi kama kanisa sasa hivi tupo jangwani (safarini), kuelekea nchi ya ahadi ya kaanani ambayo ni Mbingu mpya na nchi mpya, na katikati ya safari yetu hii Mungu anatujaribu na kutupima uthabiti wa imani zetu kwake, na mwenye kuvulimia hadi mwisho ndiye atakayeokoka (Mathayo 24:13), hivyo, tutakapomaliza safari yetu ya imani katika Kristo tutakuwa tumemaliza majaribu ya dunia hii kama wana wa Israeli walivyomaliza miaka yao arobaini na kuiingia nchi ya ahadi.


ANGALIZO: Namba arobaini na zinginezo hazina upekee wo wote ule (yaani hazina u-special wo wote ule), kwa sababu haziwezi kukuokoa na Jehanam ya moto. Kama hujatubu dhambi zako na kubatizwa kwa jina la Yesu Kristo na kufuata maagizo Yake yaliyohubiriwa na mitume na manabii Wake watakatifu sehemu yako ni katika moto wa milele.

Ufunuo 21:8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili. 

Hivyo fanya uamuzi sasa kuitii injili ya Kristo maana Yu karibu.

Marko 1:14 Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, YESU AKAENDA GALILAYA, AKIHUBIRI HABARI NJEMA YA MUNGU

15 AKISEMAWAKATI UMETIMIANA UFALME WA MUNGU UMEKARIBIATUBUNINA KUIAMINI INJILI

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Je! matumizi ya mimea ya asili kwa matibabu ni dhambi kwa mkristo?


LAKINI KWA NENO LAKO NITAZISHUSHA NYAVU.


Je! ni kweli karama ya kunena kwa Lugha haikupewa kipaumbele na mtume Paulo kama yafanyavyo baadhi ya makanisa leo hii?


MAOMBOLEZO YA ROHO KWA KANISA.


KWANINI MAKUHANI WALIAMRIWA KUTWAA MKE MWANAMKE AMBAYE NI BIKIRA TU? (Walawi 21:14)


JE! NI DHAMBI KWA MWANAMKE NA MWANAMUME KUISHI PAMOJA PASIPO KUFUNGA NDOA KIBIBLIA?

LEAVE A COMMENT