Pishi na Kiango ni Nini (Mathayo 5:15)?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

Bwana Yesu  kuna jambo alilikusudia hapa  lifahamike na  ndio maana  akatoa mfano huo katika  kitabu cha Mathayo 5:15, lakini kabla ya kuendelea mbele embu tutazame kwanza nini maana ya maneno hayo, Kiango na Pishi

KIANGO

Kiango ni kifaa maalumu kinachotumika kushikilia  au kuning’inzia taa  kwa jina lingine kinaitwa kinara, na kifaa hiki huwa lazima kikae sehemu iliyo inuka juu kidogo, ili kusaidia mwanga wa hicho kilichowekewa  juu yake yaani (taa) iweze kumulika  mahali pote

Na PISHI

Ni kibakuli kidogo au kapu dogo

 ambacho haswa watu wa agano la kale walikitumia kama kipimo cha kupimia nafaka 

Soma

Kutoka 16:18

[18]Nao WALIPOIPIMA kwa pishi, yeye aliyekuwa ameokota kingi hakubakiwa na kitu, na yeye aliyekuwa ameokota kichache hakupungukiwa; wakaokota kila mtu kama ulaji wake ulivyokuwa.

Ndiyo maana hapo Bwana Yesu anasema je inawezekana kuwasha taa na kuiweka kwenye pishi… Ni jambo ambalo haliwezekani maana ikiwa mtu ataweke chini hicho kibakuli ni wazi kabisa mwanga hautapatikana…kutakuwa giza tu.

Pia maneno haya pishi na kiango  yamejitokeza katika vifungu mbalimbali  ambavyo unaweza  kukutana navyo.

Mfano

Mathayo 5:15

Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. 

Luka 8:16

Hakuna mtu ambaye akiisha washa taa huifunika kwa chombo, au kuiweka mvunguni, bali huiweka juu ya kiango, ili waingiao wapate kuona nuru yake. 

Ni jambo gani Bwana wetu Yesu Kristo alitaka tulielewe kuhusu maneno hayo, moja kwa moja Bwana Yesu kuna kundi alililenga ili lipate kufahamu, na kundi lenyewe ni watu waliomwamini Yesu Kristo, watu wengi wamekuwa wakidhahania kuwa ukisha mkiri Yesu Kristo ukiwa ndani ya wokovu basi wamemaliza, lakini haipo hivyo ndiyo maana Bwana alitoa mfano je mtu anaweza kuwasha taa na kuweka chini pishi, yaani mfano uwashe taa yako kisha uiweke chini ya uvungu wa kitanda ni jambo ambalo haliwezekana

Sasa hicho ndicho Bwana alikimaanisha kwa waliomwamini Yesu,    

Kuwa yeyote aliyeokoka hapaswi kuuficha wokovu wake bali anapaswa  aunganze kwa watu wote Ndio maana ukiendelea katika hiyo Mathayo 5:16 inasema

Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni. 

Matendo yako wewe uliyeokoka yanapaswa yahubirie watu wengine ili kwamba na wengine  wavutwe kupitia wewe 

Ikiwa umemwani Yesu Kristo na bado matendo yako yanamwakilisha baba wa uongo shetani, hapo ni sawa na umewasha taa kisha ukaiweka chini ya uvungu wa kitanda chako, uwezi sema umeokoka halafu ulevi wewe, wizi wewe, uzinzi ni wewe, uongo wewe,  na mambo yafananayo na hayo yanakuwa ndani yako hapo jua kabisa siyo tu umeiwasha taa yaani hapo jihesabie  kuwa umeizima kabisa..

Hivyo basi lazima tujionyeshe kuwa tumebadilishwa na Yesu Kristo lazima matendo yetu mema ambayo tunayapata kwa Bwana wetu ambaye ndiye kielelezo chetu  basi na tutende ishi maisha ya kumpendeza Mungu  hili kupitia wewe watu waokolewe, 

Je matendo yako yanamhubiri Yesu Kristo

 jibu unalo wewe 

Nuru yako iokoe watu 

Ubarikiwe

Kwa mawasiliano zaidi +255693036618/+255789001312

Jiunge pia na Channel yetu ya  WhatsApp. 

“ NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

LEAVE A COMMENT