Nini maana ya kupanua hirizi, na kuongeza matamvua?

SWALI: Nini maana ya Mafarisayo hupanua HIRIZI zao na kuongeza MATAMVUA yao? na ni kwa namna gani, wameketi katika kiti cha Musa? (Mathayo 23:1-5)

JIBU: Nakusalimu kwa jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo nakukaribisha katika kuyatafakari maneno ya uzima.

Kabla ya kwenda moja kwa moja katika jibu ni vyema tufahamu mafarisayo ni watu gani??

MAFARISAYO walikuwa ni viongozi wa kidini katika taifa la Israeli, walikuwa ni watu wenye elimu kubwa yaani wasomi, katika maswala ya Torati ya Musa. Na maana halisi ya jina lao ni (waliojitenga na Wakosefu.) ili kushika kiaminifu masharti yote ya torati ya Musa.

Mathayo 23 :1-3  Kisha Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake, akasema, Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa;basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi.

Ukisoma hapo juu utaona ni sababu gani Bwana Yesu alisema hivyo (Mathayo 23:3”……MAANA WAO HUNENA LAKINI HAWATENDI).

Hiyo ndio sababu ambayo aliwaambia wanafunzi wake wasitende matendo kama yao. Yaani wasifuate mwenendo wa mafarisayo bali wasikilize tu kile wanachofundishwa (maana ni torati na si maneno yao) na wayatendee kazi lakini wasifuatishe matendo yao ama tabia zao.

Pia aliposema Mafarisayo na Msadukayo wameketi katika kiti cha Musa (Mathayo 23:2” Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa;”).

Maana yake ni kwamba hawa Mafarisayo na Masadukayo. Walikuwa wanaifahamu sana Torati ya Musa. Na ilikuwa ni rahisi sana kwao kutumia Torati ya Musa katika kuhukumu. Kupitia hiyo torati ya Musa. Hivyo jambo lolote likitokea katika Israeli wao ndio walikuwa ni watoa hukumu kulingana na Torati inasema nini Kama jambo likitokea,

 Ilihali na wo pia sirini wanafanya hivyo hivyo na walistahili hukumu kama wanayawatolea watu wengine. 

Walikuwa ni wepesi wa kuhukumu ingali nao ni watenda maovu vivyo hivyo.

Yesu alisema pia..

Yohana 8:7” Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.” 

Ukisoma hapo utaona hakuna aliyemrushia jiwe Yule mwanamke kwa kosa alilolifanya, maana dhamiri zao ziliwashuhudia kuwa wao nao ni watenda maovu ni wazinzi kama huyo walietaka apigwe mawe mpaka kufa. Maana nao walitakiwa wapigwe mawe hivyo hivyo.

Sasa aliposema “wanapanua hirizi” zao

(Mathayo 23:5”  Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao;”)

Hapa hakuwa na  maana ya Hirizi tunazozifahamu wanazotumia waganga na wachawi sivyo.

Kwa kiingereza ni “PHYLACTERY” yaani ni kibox kidogo kilichobeba maandishi ndani yake ambacho walikuwa wakitembea nacho kama kumbukumbu kila sehemu wanakokwenda ili wasisahau kile wanachotakiwa kukifanya ama kukikamilisha katika maisha yao kuhusu Mungu, 

Mfano mtu anaeweka kengele ya saa ya kumkumbusha jambo la kufanya muda Fulani ukifika, Ikiwa atasahau basi kengele aliyoweka italia na atakumbuka anatakiwa afanye nini.

Haukuwa ni utaratibu tu waliojiwekea wao bali wana wote wa Israeli waliamuliwa kufanya hivyo na Mungu mwenyewe. Waandike baadhi ya vifungu maalumu vile vya muhimu zaidi alivyoagiza Mungu. kisha wawe wanatembea navyo popote wanapokwenda. Wavivae kama utepe katika macho yao lakini pamoja na katika mikono yao. Ndio vikawa vinaitwa hirizi.

Tunalidhibitisha hilo tukisoma

Kumbukumbu la Torati 6:4-8” Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja.Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;  

nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako.”

sasa badala ya kutengeneza kiboksi kidogo tu mfano wa nchi 2 au tatu, wao Mfarisayo walizidisha kikawa si kibox kidogo tena likawa  ni “li-boksi” ili waonekane na watu kama jina lao lilivyo “walojitenga na wakosefu” yaani watakatifu sana kuliko wengine.

Pia hata matamvua yalibidi yawe ya kawaida tu ila wakayaongeza pia na hayo. 

Matamvua kwa wayahudi ni sehemu ya mwisho kabisa ya kanzu wanazovaa katika sehemu za mikono,  Mungu aliamuru wazishone wakizichanganya na michiri ya rangi ya samawi(BLUE) sasa wao waliyashona yakawa ni mkubwa zaidi.

Hivyo kila kitu wao walifanya kukiongeza zaidi matamvua lakini pamoja na hirizi(kibox) lengo lao waonekane wasafi yaani watakatifu sana na washika sheria kwa uaminifu kabisa.

NINI TUNACHOJIFUNZA KATIKA JAMBO HILI?

Hii inafunua dhahiri kuwa baadhi ya viongozi wa kanisa hili la laodikia (kanisa la Mwisho) wanavaa majoho makubwa pamoja na misalaba mikubwa,  ili kujionyesha mbele za watu kuwa wao ndio waliokubaliwa na Mungu ni wataratibu katika ibada zao na mambo mengi. Lakini nia yao kubwa haswa ni kuheshimiwa wao na sio Kristo katika kanisa hii ni hatari kubwa mno.  

Maana nia yao ni kuonyesha ukubwa/vyeo na mamlaka yao. Lakini ndani yao hawana tofauti na Mafarisayo maana hawayashiki yale wanayoyasema ni WANAFIKI.

Ubarikiwe sana Bwana YESU.

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu.

Je! Umeokoka? Kama bado unasubili nini ndugu yangu? Tenegeneza mambo yako sasa maaana bado mlango wa neema uko wazi. Wala hujachelewa leo ni mzima kesho hujui kama utakuwa mzima usiishi kwa kubahatisha ikishi katika tumaini la kweli katika Kristo Yesu.

Nuru yako iokoe watu 

Ubarikiwe

Kwa mawasiliano zaidi +255693036618/+255789001312

Jiunge pia na Channel yetu ya  WhatsApp. 

“ NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Masomo mengine:

NAO WALIOPOKEA NENO LAKE WAKABATIZWA.

WOKOVU HAUKAMILISHWI KWA TENDO MOJA HALAFU MENGINE UKAYAACHA

JE! NI KWELI MARIAMU MKE WA YUSUFU NI MALKIA WA MALAIKA, MANABII, MITUME, NA WATAKATIFU WOTE?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *