DUMU KATIKA FUNDISHO LA MITUME.

Jina la Bwana Wetu na Mungu Wetu Yesu Kristo lihimidiwe milele na milele. Amina. 


Ikiwa umeshampa Kristo maisha yako kwa kutubu dhambi zako kwa kudhamiria kuziacha  na kubatizwa katika ubatizo sahihi, basi tambua kuwa, hiyo ni hatua ya awali kabisa katika safari yako ya wokovu wa nafsi yako, lipo jambo jingine muhimu sana baada ya hilo, nalo si jingine zaidi ya KUDUMU KATIKA FUNDISHO LA MITUME.


Siku ile ya pentekoste baada ya watu kisikia mahubiri ya Petro, biblia inasema kuwa, watu wale waliomini walibatizwa kwa JINA LA YESU KRISTO siku ile ile (kama ulibatizwa kwa jina la Baba, Mwana na Roho fahamu kuwa huo ni ubatizo feki kama zilivyo imani nyingine feki) ubatizo sahihi na wa kimaandiko ni wa kizamishwa katika maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo..

Matendo Ya Mitume 2:37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

 38 Petro akawaambia, Tubuni MKABATIZWE KILA MMOJA WENU KWA JINA LAKE YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 

Watu hawa baada ya kuamini na kubatizwa, waliachana na mafundisho yao ya awali waliyokuwa nayo huko kabla, na pia, hata wale wa madhehebu ya mafarisayo na masadukayo walioamini, waliachana na mafundisho yao ya awali na KUDUMU KATIKA FUNDISHO LA MITUME.

Matendo Ya Mitume 2:42  WAKAWA WAKIDUMU KATIKA FUNDISHO LA MITUME, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali. 

Ndugu, ikiwa na wewe umeshampa Kristo maisha yako na kupokea Roho Mtakatifu, basi huna budi kuachana na mafundisho ya awali ya mila zako za uchawi, uganga, unywaji pombe na kafara za mababu na mizimu na udumu katika fundisho la mitume, achana na mafundisho potofu ya dhehebu lako ya ubatizo wa vichanga, kuwaomba marehemu, kufundishwa kunena kwa lugha, kuruhusu wanawake kuwa  wachungaji na yote yaliyokinyume na biblia na dumu katika Fundisho la mitume, achana na mafundisho ya awali ya huyo nabii wako, mchungaji wako na askofu wako kuwa, Mungu anatazama roho, hivyo vaa vimini, nusu uchi na suruali, weka nywele bandia, makeup kucha bandia haina shida,  achana na hayo mafundisho na dumu katika fundisho la mitume kwa kusoma biblia yako ili ufahamu mitume walihubiri nini kwani Mungu atakuhukumu kulingana na injili yake iliyo hubiriwa na mitume wake.

Warumi 2:16 katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu.

Bwana akubariki, Shalom.

Maran atha!


Mada zinginezo:

INJILI YA KRISTO HAIENDI NA WAKATI


Siku sahihi ya kuabudu ni ipi, siku ya sabato ni lini?


Je! Ni kweli Bwana Yesu alishika sabato kuninganana luka 4:16?


Biblia imeruhusu ubatizo wa vichanga? (kulingana na matendo 16:33)


Je! Kuna Mungu wawili? (Kulingana na Yohana 1:1)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *