Shalom nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.
Ni kawaida moyo wa Mwanadamu kuugua pale kitu alichotarajia kukipata kikikawia, huenda kwa kuahidiwa na mtu kupewa jambo fulani ama kuahidiwa na Mungu kuwa atapewa jambo fulani pale hicho kitu kinapokawia kuja moyo wake huugua.
Maandiko yanasema.
Mithali 13:12 “Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima”.
Lakini maandiko yanasema “…Bali haja ya mtu ikipatikana, ni MTI WA UZIMA.” unaona hapo!, Sasa ni kwa namna gani mti wa uzima?
Maandiko yamesema mara kadhaa juu ya Mti sasa je ni mti kama mti unaozungumziwa jibu ni la!, Bali mti unafananishwa na Mtu katika maandiko.
Marko 8:24 “Akatazama juu, akasema, Naona watu kama miti, inakwenda”.
Ili tuelewe vyema tusome pia..
Luka 6:44 “kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu.
45 Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake”.
Kama Mtu ni mwema Mtakatifu aliesamehewa dhambi na kuyaishi maandiko huyo mtu ni MTI WA UZIMA! Kile kitakachotoka ndani yake yaani matunda yatokanayo na Msamaha wa dhambi yatawapa uzima wengine pia anapowashuhudia Habari za Kristo na jinsi mwenendo wake ulivyo tofauti na wengine ambao hawajamuamini Kristo bado.
Hata watu ambao wamefanikiwa kupata kile wanachokihitaji huwa wanafuraha na unaweza kuwauliza jambo lolote wakakujibu vizuri na kwa ufasaha maana wanafuraha ndani yao.
Utaona maneno mazuri wanatamka vinywani mwao.
Mithali 15:4 “Ulimi safi ni mti wa uzima;
Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo”.
Tofauti na mtu ambae kile anachokitarajia kimekawia(hajakipata bado)
Anakuwa ni mtu ambae hata ukimuuliza usitegemee kupata jibu lililonyooka kabisa atakujibu shortcuts tu atakuwa ni mkali nk.
Hivyo pia sisi tunapompokea Roho Mtakatifu kwa kumpa kwanza Yesu Kristo maisha yetu tunakuwa na Furaha na Amani ndani yetu,tunakuwa ni mti wa uzima ghafla kutoka katika huzuni, Mateso mauti tunakuwa mti unaotoa matunda yenye uzima maana mti hutambulikana kwa matunda yake.
Hivyo na sisi tutaanza kutambulika kwa matunda yetu.
Mithali 3:13 “Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu.14 Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.
15 Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye.
16 Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.
17 Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani.18 Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu ashikamanaye naye”.
Ikiwa hujampokea Yesu Kristo basi wewe si mti wa uzima wala huwezi kutoa matunda ya uzima, mpe leo Kristo maisha yako haya matunda yatatoka yenyewe tu maana Kristo ndio anaeishi ndani yako hakuna namna yoyote yanaweza yasitokee.
Ubarikiwe sana.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.