JE KUNA TOFAUTI GANI KATI YA MADHABAHU NA MIMBARI?

  Uncategorized

Jina la mwokozi wetu Yesu kristo lihimidiwe daima.

Karibu tujifunze maneno ya uzima.

Je madhabuhi ni nini?

Madhabahuni ni eneo la kanisa ambalo watu wote uenda na kumtolea Mungu sadaka , kuomba, kushiriki meza ya Bwana, na kupeleka shukrani za sifa kwa Mungu (ni mahali pa kukutana na Mungu).

Kwa maana hiyo madhabahuni si pale mbele ya kanisa tu, bali ni lile eneo lote la ndani ya kanisa, pale mbele huwa panasimana tu kama kitovu cha madhabahu Yote..

Na Mimbari ni nini?

Mimbari ni lile eneo la mbele lililoinuka, ambalo limetengwa rasmi kwa ajili ya Neno la Mungu kuhubiriwa au taarifa za kikanisa kuwasilishwa, au huduma nyinginenyingine

za kiibada kutendeka kama vile uimbaji wa kwaya.

Lakini haya maneno mawili huwa yanatumika kutokana na uelewa wa mtu, mwingine utasikia anasema nakwenda madhabahuni kuhubiri mwingine atasema nakwenda mimbarini, lakini wote wawili hawajabadili maana, kwasababu mara nyingi mimbari huwa pale pale madhabahuni.

Hivyo ikiwa mtu anaenda kuhubiri, kuhutubu, au kuimba kwaya kiuhalisia mtu huyo ni sawa na anasimama mimbarini, lakini ikiwa anakwenda kwaajili ya kuomba, kutoa sadaka, kufanya ibada ya kusifu na kuabudu, hapo haisogelei mimbari bali madhabahu ya Mungu.

Mimbari ni mahali pa kusikilizwa, lakini madhabahuni, ni mahali pa kushiriki.

Bwana akubariki.

Je!, umeokoka, kama bado bado nafasi unayo mpe leo Kristo maisha yako utue mizingo yako yeye ameshalipa deni yako yote fungua moyo wako tu.

Bwana Yesu akubariki sana.

Tafadhali washirikishe na wengine ujumbe huu wasiliana nasi.

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312.<< NINI MAANA YA KUVUKIZA UBUMBA.

LEAVE A COMMENT