NINI MAANA YA KUVUKIZA UVUMBA.

Uncategorized No Comments

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo Mwokozi wetu.

SWALI: KUVUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE?

UVUMBA kwa Jina jingine ni UBANI. Ni mchanganyiko wa viungo mbali mbali ambao huchangwanywa pamoja na baada ya kukamilika huchomwa na kutoa harufu nzuri.

Hivyo Uvumba ni Manukato yenye harufu nzuri sana pale unapochomwa katika Moto. Chanzo kikubwa cha uvumba kinapatikana katika miti ya Boswellia na thurifera. Miti hii hupatikana katika nchi ya Yemeni na nchi jirani.

Tukirudi katika biblia hasa katika Agano la Kale, Mungu aliwapa maagizo wana wa Israeli kabla hawajafika kwenye ile nchi ya Ahadi,  Kaanani. Walipokuwa bado wako jangwani, tunafahamu Mungu aliwaambia watengeneze hema ya kukutania, na si hivyo tu bali aliiwambia pia watengeneze UVUMBA ambao huo makuhani peke yao ndio watakaokuwa wakiingia watakuwa wakiuchoma kila siku ndani ya hiyo hema walio agizwa kuitengeneza.

Sasa waliokuwa wanaruhusiwa kufanya kazi hii ya kuvukiza uvumba ilikuwa ni Makuhani peke yao na si Mtu mwingine. Na ilikuwa ni Amri ya daima ilikuwa ni lazima kila siku wafanye hivyo ndani ya ile hema ya kukutania.

Katika ile madhabahu ile ndogo iliyokuwa ndani ya hema ya kukutania.

Pia Bwana aliwaambia wana wa Israeli,  wasitengeneze Uvumba kwa viongo vile vile kwa ajili ya matumizi yao wenyewe. Viungo hivyo vya kutengenezea uvumba pamoja na kanuni/formula ya kutengeneza kwa ajili ya Bwana tu. Na si vinginevyo.

Tunalidhibitisha hilo tukisoma.

Kutoka 30:34 “Bwana akamwambia Musa, Jitwalie MANUKATO MAZURI, yaani, natafi, na shekelethi, na kelbena; viungo vya manukato vizuri pamoja na ubani safi; vitu hivyo vyote na viwe vya kipimo kimoja;

35 nawe UTAFANYA UVUMBA WA VITU HIVYO, manukato ya kazi ya ustadi wa mtengenazaji manukato, yatakuwa yamekolea, safi, matakatifu;

36 nawe baadhi yake utayaponda sana, na kuyaweka mbele ya ushuhuda ndani ya hema ya kukutania, hapo nitakapokutana nawe; nayo yatakuwa kwenu matakatifu sana.

37 Na uvumba utakaofanya, hamtajifanyia uvumba wenye viungo sawasawa na uvumba huo; utakuwa kwenu mtakatifu kwa ajili ya Bwana”.

NI KWA NINI BWANA ALIWAPA MAAGIZO YA KUVUKIZA UVUMBA KATIKA NYUMBA YAKE?, YAANI HEMA YA KUKUTANIA.

JIBU:  Tukisoma agano la Kale ni kivuli cha Agano Jipya tulilonalo sasa, hivyo katika agano la Kale lugha ya maumbo/picha ilikuwa ikitumika kuwakilisha mambo halisi yanayotendeka katika ulimwengu wa Roho.

Kama tu tunavyosoma kuhani Mkuu alivyokuwa akiingia mara moja kwa ajili ya upatanisho wa dhambi za taifa la Israeli alipokuwa akiingia na damu ya Mwanakondoo.

Katika ulimwengu wa Roho ilikuwa ikimuwakilisha Mwoko wetu Yesu Kristo ambaye aliingia patakatifu pa patakatifu kwa Damu yake mwenyewe si ya kondoo tena, akitupatanisha sisi na Mungu, na ameingia Mara moja tu na kutupatanisha sisi na Mungu yeye aliekuhani Mkuu. Na tumefanyika wana wa Mungu kupitia damu yake na kusamehewa deni ya dhambi pale tunapomuamini, tukumbuke zamani dhambi zilikuwa zikifunikwa tu baada ya mwaka zinakumbukwa tena sasa kupitia Kristo Yesu Bwana wetu tunasamehewa milele wala yeye mwenyewe ameahidi dhambi zetu hatazikumbuka tena. Kwa damu ya thamani iliyomwagika pale Kalvari HALELUYA.

Hivyo mambo yaliyokuwa yakifanyika katika Agano la Kale yote yalikuwa yanafunua mambo dhahiri katika agano jipya.

Soma Waebrania 4:14-16.

Vivyo hivyo ule Uvumba uliokuwa ukichomwa katika ile hema ya kukutania ulikuwa ukiwakilisha katika agano jipya jinsi maombi ya watakatifu yanavyopaa mbele za Mungu kama harufu nzuri ya manukato HALELUYA!!

Na tunaona Mungu aliwapa maagizo watengeneze kwa viungo vipi na vipi, pia inafunua kwetu tunapoomba sawa na Neno lake maana yake maombi yetu yanakuwa ni halafu nzuri mbele za Mungu.

Na ndio maana Daudi anasema katika.

Zaburi 141: 2 “SALA YANGU IPAE MBELE ZAKO KAMA UVUMBA, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.”

Daudi alionyeshwa jambo hili mapema na ndio maana akawa ni mtu wa kumsifu Mungu kila kukicha alikuwa anajua ni kipi anachokifanya.

JE!, NA KATIKA AGANO JIPYA TUNACHOMA UVUMBA?.

Tumeshakwisha kupata ufunuo uliokuwa katika kuchoma UBANI ilikuwa ikiwakilisha Mambi ya watakatifu,  jinsi yanavyoleta harufu nzuri mbele za Mungu wetu.

Hivyo katika agano jipya Uvumba wetu/ubani wetu ni maombi yetu sisi watakatifu tuliomuamini Kristo Yesu!  HALELUYA HALELUYA.
Tuwe ni watu wa kuomba kila siku mbele za Mungu. Kumbe maombi yetu ni harufu nzuri mbele za Mungu wetu.

Tunalidhibitisha hilo katika kile kitabu.

Ufunuo 5:8 “ Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, NA VITASA VYA DHAHABU VILIVYOJAA MANUKATO, AMBAYO NI MAOMBI YA WATAKATIFU.”

Ufunuo 8:4 “NA MOSHI WA ULE UVUMBA UKAPANDA MBELE ZA MUNGU PAMOJA NA MAOMBI YA WATAKATIFU, kutoka mkononi mwa malaika.” 

Sasa Shetani naye hayuko nyuma kuhakikisha anaendelea kuwadanganya watu, leo utasikia watu wanaambiwa wachome udi majumbani na makanisani katika biashara nk. Ili kufukuza Roho chafu yaani mapepo ndugu usidangayike hizi ni siku za Mwisho. Uvumba pekee unaoweza kufukuza roho chafu nyumbani, kazini katika biashara, makanisani nk ni MAOMBI YAKO WEWE MWANA WA MUNGU.
Hakuna Uvumba wenye nguvu zaidi kama MAOMBI,

Wala usidanganyike kuwa damu ya mbuzi na kondoo na ng’ombe zinaondoa mikosi na kukupa baraka ndugu huo ni UONGO wa Shetani,  usisikilize kabisa damu pekee iwezayo kuondoa mikosi, laana,nk ni ya YESU KRISTO TU. ndio ndio iletayo uzima si uzima tu bali uzima wa MILELE na TUMAINI uhakika.

Je!, umempa Bwana Yesu Kristo maisha yako?, kama bado unangoja nini? Kesho si yako hujui yatakayokuwako!, usalama uko katika Kristo Yesu hizi ni nyakati za Mwisho, isalimishe roho yako kwa Mwokozi pekee Kristo Yesu.

Ubarikiwe sana.

Tafadhali shirikisha ujumbee huu na wengine.

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *