NINI MAANA YA KARISMATIKI?

Maswali ya Biblia, Uncategorized No Comments

Karismatiki. Ni neno la Kigiriki “Charisma ” lenye maana ya Favour(Upendeleo) au Gift (zawadi). Charis(Grace) yaani Neema. Hivyo tunaweza kusema kwa Lugha nyepesi ni

zawadi au uwezo anaopewa mtu binafsi na Roho Mtakatifu kwa manufaa ya Kanisa au ukuaji wake wa kiroho.

Ni jambo ambalo lilianza Mwanzoni kabisa Mwa karne ya ishirini (20) mnamo Mwaka 1906 nchini Azusa Marekani,  na baadae kikasambaa katika Ulimwengu wote na katika madhehebu mbali mbali.  Kama vile Lutherani(1962), Roman Catholic(1967) nk. Ni neno ambalo utalisikia likitajwa sana.

Kanisa la Pentekoste lilianza katika miaka ya 1906 ambapo liliamini kuwa nguvu za Mungu ama udhihirisho wa Mungu kuwepo katikati ya wanadamu, ambazo ndizo karama za Roho Mtakatifu tunazozisoma.
1 Wakorintho 12.

Kanisa hili la Pentekoste baadhi ya watakatifu waliokuwa tayari walikaa kumuomba Roho Mtakatifu wakitaka hizo nguvu zidhirike ndani yao maana jambo hilo lilikuwa katika kanisa la kwanza la Mitume na baada ya hapo, iliaminika kwa kipindi kilefu sana kuwa jambo hilo halipo tena.

Ila watakatifu hawa walioba si sawa ikabidi wafunge na kuomba ili karama za Roho Mtakatifu zidhihirike ndani yao kama kunena kwa Lugha, kutoa unabii nk. Na kweli jambo hilo kwa uwezo wa Roho Mtakatifu likadhirika.

Ni kitu ambacho kilionekana ni kigeni na nicha ajabu kwa makanisa ya zamani yaliyokuwepo, kama Pentekoste, Anglikana, Roman Catholic nk.

Hivyo jambo hili liliendelea kwa kasi mpaka mwaka 1980 baadhi ya madhehebu makongwe yakaanza kuurithi mfumo huo ikiwemo Roman Catholic(RomanCatholic karismatiki), Lutherani na mengine mengi.

Japo kuwa misingi ya imani ya makanisa haya imepishana.

Hivyo kanisa lolote ambalo linaamini karama za Roho Mtakatifu na linasisitiza hivyo katika mafundisho yake basi hilo kanisa tunaweza kuliita ni Kanisa la Karismatiki.

NI KIPI TUNACHOTAKIWA KUFAHAMU KATIKA VIPAWA HIVI VYA ROHO MTAKATIFU (KARISMATIKI, “Gift/favor  of Grace).

Kanisa lolote lisilokuwa na udhihirisho wa nguvu za Mungu kama kunena kwa Lugha, uponyaji,unabii, nk watu wanamuabudu tu Mungu na kusikiliza neno kisha wanaondoka kama walivyoigia siku zote hakuna mguso wa Roho Mtakatifu wala vipawa havidhiriki hilo kanisa halina uzima. Yaani ni kanisa lililokufa.

Maana Mungu si mbinafsi kwamba apogee tu maombi na sifa anazoimbiwa na watoto wake halafu yeye asitoe vipawa vya kuwafaidia watoto wake na kanisa. Haiwezekani Mungu hayuko hivyo kabisa.

Pia Shetani hujigeuza kuwa kama malaika wa Nuru lakini sivyo. Watu wengi wanapokea roho zingine nazo zinanena vile vile lakini mambo wanayoyatenda ni maovu. Hivyo nikuwa makini sana katika nyakati hizi za Mwisho.

NI KIPI TUNACHOTAKIWA KUFANYA SISI WANA WA MUNGU?

Katika nyakati hizi za Mwisho akili zetu,fahamu zetu tuzielekezee zaidi katika Neno la Mungu yaani Biblia,katika kila jambo tunalofanya ama tunaloambiwa kufanya ikiwa ni manabii wetu,Wachungaji wetu tusikubali tu na kutekeleza pasipo kuhakikisha kuwa kile tunachoambiwa je? Kinakizana na Neno la Mungu ama hakikinzani ikiwa kinakinzana na Maandiko kitupe kando kabisa haijalishi atakuwa amesema nani hata kama ni Malaika ikiwa kinakinzana na maandiko usikitekeleze kabisa zama hizi ni za uovu.

Ikiwa kweli umempokea Roho Mtakatifu,  tambua ni lazima kunabadiliko lazima lionekane ndani yako. Huwezi ukaendelea tena kuabudu sanamu, ama kupekeka maombi yako kupitia Mtakatifu Fulani wakati tumeambiwa lolote tuombalo na tuombe kwa Jina la Yesu tu. Wala si kupitia kitu kingine ukiona mambo kama hayo yanaendelea hatakama huyo mtu ama wewe mwenyewe unanena kwa Lugha, unatoa unabii,unaimba nk ndugu fahamu huyo si Roho Mtakatifu.

Roho Mtakatifu siku zote anatuongoza katika kweli yote hawezi kuendelea kutuacha katika upotevu HAIWEZEKANI.

Usipende kusikiliza kila siku Nabii fulani ama mchungaji fulani, ama Askofu fulani, au papa fulani au Padri fulani kasema hivi na unaamini hutakii kusoma neno na kumuomba Roho Mtakatifu akufundishe ndugu Shetani yupo kazini jilinde kwanza mwenyewe kabla ya kulindwa na wengine.

1Yohana 4:1  “Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani”

Je!, umeokoka, kama bado bado nafasi unayo mpe leo Kristo maisha yako utue mizingo yako yeye ameshalipa deni yako yote fungua moyo wako tu.

Bwana Yesu akubariki sana.

Tafadhali washirikishe na wengine ujumbe huu wasiliana nasi.

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *