Nini maana ya kanisa
Zamani hata mimi kabla sijapata ufahamu/ maarifa ya maana halisi ya kanisa ipi, ukweli kabisa nilijua kuwa kanisa NI JENGO, tena na pale nilipona na msalaba basi akili yangu yote na ufahamu nikajua kanisa ni jengo ambalo bila hilo watu hawawezi kusanyika ili wamwabudu Mungu, huwenda sikua Mimi yamkini na wewe pia ulipitia sintofahamu katika hili..
Basi ipi ni maana halisi ya kanisa
Kanisa Ni Neno lililotokana na lugha ya kiyunani EKKLESIA, ikimaanisha “WALIOITWA”, na katika kipindi cha agano jipya, kusanyiko lolote la wakristo walipokusanyika kwa ajili ya kujifunza, kusanyiko hilo lilitambulika kama kanisa
Sasa hiyo ndiyo maana halisi ya kanisa yaani ni walioitwa, hivyo watu wowote ambao wamemkabidhi Yesu Kristo maisha yao yaani walio (okoka) hao moja kwa moja wanatambulika kama kanisa (walioitwa), na watu kama hao maandiko yanasema pindi tu wanapokutanika kwa ajili ya kujifunza basi Bwana anakuwa katikati yao, tunalithibitisha hili katika kitabu cha
Mathayo 18:20
Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa Jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.”
Hii ikitufundisha pia ikiwa kutatokea kusanyiko lolote, ambalo halitambui Jina la Yesu yaani hawajamkiri Yesu Kristo wala habari zake hawazijui yaani kusanyiko hilo, hata liwe lina utashi wa kuzungumza kwa namna gani kamwe Yesu anakuwa hayupo pale, na si mimi nimesema maneno hayo, lakini Yesu mwenyewe anasema
“Walipo wawili watatu WAMEKUSANYIKA KWA JINA LA LANGU nami nipo papo hapo katikati yao”
Umeona hapo anasema kwa jina lake, hapo ndipo anakuwepo kwahiyo sasa toa mtazamo wa jengo ndani ya akili yako, kisha jihoji je umeitwa, ili isije ukawa unakusanyika bure.
Ndiyo maana hata mtume Paulo alizungumza maneno haya hili kukanusha nini maana ya kanisa katika kitabu cha
Wagalatia 1:13
[13]Maana mmesikia habari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu.
Zingatia hapo alipo sema “kanisa la Mungu” ukisoma vizuri hiyo sentensi haionyeshi kama alizungumzia jengo, bali hapo anazungumzia watu walimwamini Yesu namna alivyowaudhi kwa kuwaharibu kupitia kiasi
Hivyo bado inatuthibishia kuwa kanisa ni walioitwa waliomkiri Yesu Kristo na si makanisa (majengo) yalijengwa kwa uweledi mkubwa hapana!! toa kabisa fikra hiyo.
Je? umemwamini Yesu Kristo katika maisha je wewe UMEITWA, ikiwa ulikuwa ujatambua jambo hili na kila siku ulikuwa unaenda kanisani basi sasa badili mtazamo wako, na umwamini Yesu maishani mwako, kuwa ni Mwokozi wa Maisha yako ambaye amekuita hili uzijue siri za Ufalme wa mbinguni kwa kumtumikia, basi fanya uamuzi leo.
1 Yohana 5:10-11
[10]Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe.
[11]Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe.
Ubarikiwe
Kwa mawasiliano zaidi +255693036618/+255789001312Jiunge pia na Channel yetu ya WhatsApp. “ NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>>
WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Masomo mengine
Je kujichua/ kufanya punyeto (masturbation) ni dhambi?
MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 04)