Talanta maana yake ni nini katika biblia?.

Shalom!,

Ukisoma katika Mathayo 24:14-30 utakutana na neno hili. Sasa lilikuwa likimaanisha nini?

Neno Talanta kwa Kigiriki ni “Talanton” pia kwa kilatini ni “Talentum” 

Sasa zamani hususani katika nyakati za agano la Kale Talanta kilikuwa ni kipimo cha uzito. Hasa kilikuwa kikitumika katika kupima uzito wa Madini kama Dhahabu na Shaba.

Na Talanta moja ina uzito wa kilograms 34.2

Kutoka 38:25″Na fedha ya hao waliohesabiwa, watu wa huo mkutano ilikuwa TALANTA mia, na shekeli elfu moja na mia saba na sabini na tano kwa kadiri ya shekeli ya mahali patakatifu;”

Pia ukisoma 

1 Wafalme 10:10 “Basi akampa mfalme TALANTA, za dhahabu mia na ishirini, na manukato mengi, mengi sana, na vito vya thamani; wala haukuja tena wingi wa manukato, kama hayo malkia wa Sheba aliyompa mfalme Sulemani”. 

Lakini tukirudi katika Agano Jipya talanta inatumika pia kuonyesha thamani ya fedha, au fedha yenyewe.

Talanta moja ilikuwa ni sawa na dinari 6000. Na dinari moja ni mshahara wa kibarua wa siku, labda tuseme Tsh. 15,000. Hivyo uzidisha hapo utaona jinsi fedha hiyo ilivyo nyingi sana.

Katika kisa tunachokisoma  katika Mathayo 18:21-35, tunaona kulikuwa na mtumwa aliyesamehewa talanta elfu kumi, lakini yeye akashindwa kumsamehe mwenzake aliyemdai dinari mia. Hivyo habari ilimpofikia Yule aliyemsamehe mapesa mengi, akaghadhibika na kwenda kumkamata na kumtia na yeye gerezani. Kufunua msamaha tulioupata kwa Yesu Kristo. Yatupasa na sisi tuwe watu wa kusamehe, kwasababu tuliyosamehewa na Bwana Yesu ni mengi sana,

Pia utaona talanta imetumika kama Fedha kwa yule bwana aliyesafiri akawaachia watumwa wake watatu talanta, ambapo yule mmoja alimpa talanta tano, mwingine akampa talanta mbili, mwingine akampa talanta moja. Na tunaona yule aliepewa moja alikwenda kuificha.

(Mathayo 25:15-30.).

Hivyo tunaona katika vipimo vya namna zote iwe fedha ama dhahabu kilikuwa kikitumika maana yake ni moja ya kipimo cha juu sana.

Pia talanta tunaiona katika kile kitabu cha mwisho kabisa cha UFUNUO. Ikitumika kuwakilisha tena jambo lingine ambalo si zuri sana kwa wale watu watakaopokea chapa ya mnyama.

Tukisoma utaona Kuna mvua itanyesha katika hizo nyakati za dunia hii kuharibiwa pamoja na watu waovu watakaokuwepo.

Biblia inasema mawe yatakayoshuka kutoka juu ni kama talanta maana yake wanadamu wataangukiwa na mawe hapa dunia. Yenye uzito kama wa talanta ambayo ni KG 34.2 ni hatari mno.

Ufunuo 16:20-21 “Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena.

Na mvua ya mawe kubwa sana, ya MAWE MAZITO KAMA TALANTA, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.”

Itakuwa ni siku mbaya mno na ndio maana watu wataomba milima iwaangukie iwafiche na ghadhabu ya MUNGU MWENYEWEZI. Ni kipindi ambacho usitamani kuwepo hata adui yako asiwepo maana ni kipindi kinachotisha sana kama uko nje ya KRISTO. Ama umekaa mguu nje mguu ndani mbaya sana.

Ufunuo 6:14-17

[14]Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.

[15]Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,

[16]wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.

[17]Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?”

Ni kipindi kifupi sana kilichobakia sasa haya mambo yatoke hapa, si mambo yakumuombea hata unaedhani ni adui yako yampate.

Adui yako ni Shetani wala si binadamu mwenzako. Ndugu yangu tengeneza mambo yako mapema ikiwa uko nje ya KRISTO ni  hatari sana.

Tunaona wote jinsi mambo yanavyozidi kubadilika kila siku hiyo ni kutuonesha mwisho umeshafika na unyakuo ni siku yoyote usiishi maisha ya kubahatisha ndugu hutaweza. Mambo ya rohoni yanahitajii maandalizi na sio kubahatisha.  Anza kujiandaa unaposoma ujumbe huu. Na ikiwa Kuna mahali hujaweka sawa na Kristo huu ndio muda muafaka wa kufanya maamuzi maana kesho ni ya Mwokozi, leo ni yako fanya maamuzi sahihi wakati huu, Kristo anakupenda sana zaidi ya unavyofikili wala hataki uangamie ama uokoke kama yule mwizi pale msalabani ukawe mtu wa kawaida tu kule mbinguni.

Anataka uwe mwenye mamlaka. Hakuna faida yoyote katika uovu Badilika sasa.

Ubarikiwe sana.

Tafadhari share ujumbe huu na watu wengine.

Kwa mawasiliano zaidi +255693036618/+255789001312

Jiunge pia na Channel yetu ya  WhatsApp. 

“ NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Masomo mengine:

Kibanzi na Boriti kwenye biblia vinamaanisha nini?

Je kujichua/ kufanya punyeto (masturbation) ni dhambi?

Arabuni maana yake ni nini? ( Waefeso 1:14)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *