Kibanzi na Boriti kwenye biblia vinamaanisha nini?

Shalom..

Boriti ni Kipande kikubwa sana cha mbao,kipande hicho kinaweza kuwa Kwa muundo wa ki-gogo,au mbao yoyote yenye upana..

Na Kibanzi ni kichembe kidogo sana kama mchanga,wakati mwingine kufikia kuwa kama vumbi la mbao ambalo kuonekana kwake ni kugumu.ndicho Kibanzi..

Bwana Yesu alitoa mfano huo ili kuweka msisitizo kile alichotaka kuzungumza, Katika hali ya kawaida kama huwezi kuona nguzo iliyosimama mbele ya macho yako inayokuzuia usione kabisa, utaonaje vumbi la mbao lililo katika jicho la mwenzako…..Moja kwa moja huo ni unafki

Vivyo hivyo kabla hatujawahukumu watu na kasoro zao,tujichunguze kwanza,Je?  Hayo wanayoyafanya hayapo ndani yetu na sisi? Kabla hujamwambia mtu acha uwongo, Je? na wewe husemi uwongo?, Kama sivyo heri unyamaze tu, kwasababu ukisoma mistari ya juu kidogo inasema kipimo kile tuhukumucho ndicho tutakachohukumiwa na sisi…

Mathayo 7:1 “Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.

2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.

3 Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?

4 Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?

5 Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.

Bwana atusaidie sote tuyashinde hayo.

Ubarikiwe.

Kwa mawasiliano zaidi +255693036618/+255789001312

Jiunge pia na Channel yetu ya  WhatsApp. 

“ NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Masomo mengine:

IJUMAA KUU NINI? NA NI KWA NINI IITWE IJUMAA KUU?

Kwanini Nabii Eliya alitumwa sarepta kwa mjane katika mji wa sidoni?

WOKOVU HAUKAMILISHWI KWA TENDO MOJA HALAFU MENGINE UKAYAACHA

IKAWA, MFALME ALIPOYASIKIA MANENO YA TORATI, ALIYARARUA MAVAZI YAKE.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *