Kwanini Nabii Eliya alitumwa sarepta kwa mjane katika mji wa sidoni?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

1 Wafalme 17:9   Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe. 

10 Basi, akaondoka, akaenda Sarepta; hata alipofika langoni pa mji, kumbe! Mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni; akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa. 

11 Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema, Niletee, nakuomba, kipande cha mkate mkononi mwako. 

12 Naye akasema, Kama Bwana, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe.

 13 Eliya akamwambia, Usiogope; enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao.

 14 Kwa kuwa Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Lile pipa la unga halitapunguka, wala ile chupa ya mafuta haitaisha, hata siku ile Bwana atakapoleta mvua juu ya nchi.

 15 Basi akaenda, akafanya kama alivyosema Eliya; na yeye mwenyewe, na Eliya, na nyumba yake, wakala siku nyingi. 

JIBU: Shalom, agano la kale ni kivuli cha agano jipya bali mwili ni wa Kristo, hivyo basi, kitendo hicho cha nabii Eliya kutumwa sarepta kinamfunua Bwana Yesu  mwenyewe. Soma katika

Luka 4:24   Akasema, Amin, nawaambia ya kwamba, Hakuna nabii mwenye kukubaliwa katika nchi yake mwenyewe. 

25 Lakini, kwa hakika nawaambia, Palikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita, njaa kuu ikaingia nchi nzima; 

26 wala Eliya hakutumwa kwa mmojawapo, ila kwa mjane mmoja wa Sarepta katika nchi ya Sidoni. 

Umeona hapo Bwana Yesu anajifananisha na Eliya pale alipotumwa sarepta? Hii ni kufunua nini sasa? Ni kufunua kwamba mimi na wewe ndio huyu mwanamke mjane na Eliya ni kama Bwana Yesu. 

Sasa utagundua kuwa Eliya alipofika kwa huyo mjane alitaka kwanza yeye ndio awe wa kwanza kuthaminiwa harafu vitu vingine ndio vifuate, hii ni kufunua kuwa Bwana Yesu anapokuja katika maisha yetu anataka yeye awe wa kwanza, anataka uache huo uzinzi unaoupa kipaumbele katika maisha yako na umuweke yeye kuwa wa kwanza tu, anataka uache hizo pesa za rushwa na umkubari yeye kwanza, anataka uache huo uchawi unaoutegemea na umtegemee yeye tu, anataka uachane na hao waganga wa kienyeji unao wategemea na umtegemee yeye tu, anataka uache hizo sigara na pombe na kujazwa Roho wake mtakatifu, na matokeo yake ni nini basi baada ya kuacha hayo yote? Ni kuwa tutapata ujira usio na mwisho yaani UZIMA wa milele.

Wakristo wengi leo hii hawataki kusikia sauti ya Bwana Yesu na kuwa watii kama huyu mwanamke mjane. Ndugu yangu mtii leo Bwana Yesu na ukamkaribishe katika maisha yako na awe wa kwanza kwani yeye mwenyewe alisema

Matayo 6:33  Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. 

Bwana akubariki. Shalom 


Mada zinginezo:

Je biblia inaruhusu kubatizwa kwa ajili ya wafu?(1Wakorintho 15:29)


Je! Ni dhambi kibiblia kuwaomba wafu (watakatifu)?


KUFANYA MATENDO MEMA HAIMAANISHI KUWA UMESHAUPATA WOKOVU


Itakuwa shida tajiri kuingia katika ufalme wa Mbinguni.


Je! Hadi sasa kuna manabii wa Mungu?

LEAVE A COMMENT