Je kujichua/ kufanya punyeto (masturbation) ni dhambi?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

Bwana Yesu anafundisha kwamba kumwangalia mwanamke kwa tamaa kunasababisha uzinzi katika nafsi. Ndio masturbation ni dhambi. Dhambi huanzia moyoni, na uasherati, kupiga punyeto, na kutazama ponografia ni matokeo ya ukosefu wa adili moyoni. Ili kuepuka dhambi hizi, mtu lazima ayakabidhi maisha yake kwa Yesu na kuamua kuanza maisha mapya ndani ya Kristo. 

Warumi 10:10 

Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.

Watu wengi hutafuta maombi ya kukomesha uasherati au kupiga punyeto, lakini hawajaazimia kufanya toba ya kweli. Biblia inasema wazinzi wote sehemu yao ni  katika lile ziwa la moto.

1 Wakorintho 7:1, inasema..

 “Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke.2 Lakini kwa sababu ya ZINAA kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe”.

Imeelezwa kwamba kila mwanamume awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe, kwa sababu ya dhana ya ZINAA (kufanya mapenzi nje ya ndoa au kabla ya ndoa).

 Lakini pia ni vema kufahamu kuwa mtu kuishi na mke/mke hakumzuii kulipuka tamaa,. Hata hivyo, hamu ya kuangalia wanawake wengine itabaki palepale ikiwa hawatabadilishwa.

Ili kuzuia tamaa kwa watu walioolewa au waseja, mtu lazima ayakabidhi maisha yake kwa Kristo kwanza na kukusudia kuacha dhambi na kumwamini Yesu Kristo. Kisha baada ya hapo Roho Mtakatifu atawasaidia kuvishinda vichochezi vya uasherati, kama vile ponografia, matusi, na mizaha isiyo na maana, na kugundua kwamba mambo haya hayawasumbui tena maishani mwao.

Je! ungependa kupokea msamaha wa dhambi? Ikiwa ni ndio basi wasiliana nasi kwa namba za simu uzionazo chini ya fundisho hili;

Ubarikiwe.

Kwa mawasiliano zaidi +255693036618/+255789001312

Jiunge pia na Channel yetu ya  WhatsApp. 

“ NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Masomo mengine:

“HUKU WAKIDHANI UTAUWA NI NJIA YA KUPATA FAIDA” MAANA YAKE NINI? (1 TIMOTHEO 6:5)

IJUMAA KUU NINI? NA NI KWA NINI IITWE IJUMAA KUU?

Nini maana ya kupanua hirizi, na kuongeza matamvua?

LEAVE A COMMENT