Nini maana ya neno Masihi?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

Masihi ni neno la kiebrania linalomaanisha “Mpakwa Mafuta,” (Ni mtu aliyeteuliwa na Mungu kwa kusudi fulani) wapo watu walioteuliwa na Mungu rasmi kuwa wafalme, hao waliitwa masihi wa Bwana , Pia wapo waliochaguliwa kuwa manabii, nao walijulikana kama masihi wa Bwana..

Maana nyingine ya neno Masihi ni “Kristo”,hivyo Katika biblia mamasihi (Makristo au watiwa mafuta) walikuwa wengi sana, lakini aliyekuwa masihi KIKWELI KWELI alikuwa ni mmoja tu! ambaye ni YESU KRISTO..

Mamasihi wengine ni Kweli walipakwa mafuta na Mungu lakini hawakuwa wakamilifu asilimia zote… Mfalme Daudi alikuwa ni masihi wa Bwana (Soma 1Samweli 16:6-13)lakini hakuwa mkamilifu asilimia zote, kwani aliua na pia alimtwaa mke wa Uria na kumfanya wake..

Vile vile Mfalme Sauli maandiko yanasema alikuwa ni masihi wa Bwana lakini tunasoma alikuja kukengeuka na kumdharau Mungu na maagizo yake..

1Samweli 24:9 “Daudi akamwambia Sauli, Kwa nini unasikiliza maneno ya watu wasemao, Tazama, Daudi anataka kukudhuru?

10 Tazama, leo hivi macho yako yameona jinsi Bwana alivyokutia mikononi mwangu pangoni, na watu wengine wakaniambia nikuue; lakini nikakuacha; nikasema, Sitaki kuunyosha mkono wangu juu ya bwana wangu; kwa maana yeye ni masihi wa BWANA”.

Soma zaidi 2nyakati 16:22

Hawa wote walikuwa ni watiwa mafuta lakni walikuwa na kasoro nyingi,  Lakini Yesu Kristo alikuwa ni mkamilifu kuliko hao wote..Kwahiyo yeye ndiye aliyetiwa Mafuta Makuu kuliko wote, ndio maana tunasema aliye Masihi peke yake ni YESU.

Waebrania 1:8 “Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.

9 Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio”.

Kwahiyo Wayahudi wote, na wasamaria wote, walikuwa wanautazamia ujio wa huyu Masihi mmoja ambaye atakuwa mkamilifu, asiyekuwa na dhambi hata moja, ambaye atawafundisha sheria za Mungu na kuwaokoa na dhambi zao.

Yohana 4:25 “Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote.

26 Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe, ndiye”

Yohana 1:40 “Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu.

41 Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo).

Huyu Masihi Yesu Kristo, alishakuja miaka zaidi ya elfu 2 iliyopita, akapaa mbinguni, na sasa yupo hai, na pia amekaribia sana kurudi. Atakapokuja hatakuja tena kwa kusudi la wokovu bali kwa HUKUMU

Je umemwamini Masihi Yesu?.. Umetii agizo lake la ubatizo?, na je umempokea Roho wake Mtakatifu.. Fahamu kuwa kama umekosa vitu hivyo vitatu, bado hujaokolewa kulingana na Neno lake. Hivyo ni vyema ukafanya uamuzi wa kumwamini na kutubu leo na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo, na mambo mengine yaliyosalia Roho Mtakatifu utakayempokea atakuongoza katika kweli yote.

Wasambazie na wengine habari hizi njema

Kwa Msaada, Maombezi
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge pia na Channel yetu ya  WhatsApp. 

“ NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Masomo mengine:

Kibanzi na Boriti kwenye biblia vinamaanisha nini?

Je kujichua/ kufanya punyeto (masturbation) ni dhambi?

Arabuni maana yake ni nini? ( Waefeso 1:14)<< KANISA NI NINI? na je linaundwa na nani?

LEAVE A COMMENT