MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 04)

  Siku za Mwisho, Uncategorized

Jina la Bwana Wetu na Mwokozi Wetu Yesu Kristo litukuzwe milele na milele, huu ni mwendelezo wa makala fupi inayoangazia makanisa na mafundisho ya uongo yanayowapoteza watu wengi  nyakati hizi za mwisho, kama hukufanikiwa kupata mfululizo wa makala hizi kuanzia sehemu ya kwanza, basi, unaweza tembelea website yetu ya www.Rejeabiblia.com au unaweza tuma ujumbe kwenda namba +255755251999 au +255625574252  ili utumiwe makala hizo zilizopita.

Hii ni sahemu ya nne (04) ya makala yetu, karibu!


KANISA KATOLIKI.

Hili ni moja la dhehebu kongwe ambalo linaaminika na wavivu wengi wa kusoma na kuchunguza maandiko kuwa, ndilo Kanisa la kwanza duniani kitu ambacho sio sahihi hata kidogo, ndugu, ikiwa na wewe ni miongoni mwa wavivu hao wa kusoma na kuchunguza maandiko, walioaminishwa kwa miaka mingi uongo huo, basi unapaswa utambue leo hii kuwa uliaminishwa kitu kisicho sahihi kwa kipindi kirefu sana, dhehebu la kikatoliki sio kanisa la kwanza, kulikuwepo na makanisa mengi sana ya Bwana Wetu na Mungu Wetu Yesu Kristo duniani kote kabla ya taasisi hiyo ya dini kuanzishwa, mfano wa makanisa hayo ni yale ya Galatia, Makedonia, na mengine yaliyokuwepo katika nyumba za watu mfano Filemoni.


Dhehebu la katoliki ni moja ya taasisi iliyofanikiwa kwa kiwango kikubwa sana kuingiza mafundisho potofu mengi sana katika imani ya kikristo, na mafundisho hayo potofu yanaonekana kama ni sehemu ya ukristo lakini sivyo bali ni ya kipagani, na mengi ya mafundisho hayo potofu yamedumu na yanafundishwa hadi leo hii na kanisa hilo na kuwapoteza watu wengi sana duniani. Moja ya fundisho potofu linalofundishwa na kanisa hilo ni hili..


MARIAMU NI KIMBILIO LA WAKOSEFU 

Mpendwa, Inasikitisha sana tena sana kuwaona watu pasipo aibu na kukosa roho ya huruma ndani yao,  wanawafundisha watu kwa nguvu na bidii zote na kuwaaminisha uongo huo kwamba Mariamu ni kimbilio la wakosefu, wewe unayefundisha watu uongo huo, tambua kwamba, siku moja Mungu atakuita katika hukumu yake na utalipa juu ya damu zote zilizopotea kwa uongo uliowaaaminisha watu hao kuwa Mariamu ni kimbilio la wakosefu, Mungu atakuuliza ni wapi Mimi niliposema Mariamu ni kimbilio la wakosefu?..Hutokuwa na cha kujibu siku hiyo ndugu, wewe mwenyewe unalifahamu hilo vizuri sana.


Mpendwa unayejiita katekista, Flateri, Shemasi, Padre, Paroko, Askofu, Kadinari, Papa n.k, tambua kuwa, utayalipa yote hayo kwa sababu, unawapotosha watu wenye nia ya dhati na Muumba wao kwa kuwafundisha na kuwaaminisha uongo huo kuwa Mariamu ni kimbilio la wakosefu, unashindwa kusimama katika kweli ya Mungu badala yake unasimama katika taasisi na dini yako, unashindwa kuwa mwanimifu kwa Mkombozi wako aliyemwaga damu yake kwa ajili yako, badala yake unakuwa mwaminifu kwa kiongozi wako na dhehebu lako hata kama likienda kinyume na maandiko, ndugu, hao viongozi wako na dhehebu haviwawezi kukupa wewe uzima wa milele, hivyo simama katika neno la Bwana na sio taasisi yako, na uwe mwaminifu hata kufa kwa ajili ya neno lake.

Ufunuo 2:10 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. UWE MWAMINIFU HATA KUFA, NAMI NITAKUPA TAJI YA UZIMA.

Lakini wewe mpendwa unayefundishwa kila siku na kuhudhuria kanisa hilo la uongo kila jumapili, unashindwa kabisa kujiuliza katika akili yako kuwa, mtu aliyemwamini Yesu Kristo na kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu kama wakristo wengine (Mariamu), anawezaje kuwa kimbilio la wakosefu? Au Je! Mariamu alikufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu hadi awe kimbilio lao?..unashindwa kabisa kujiuliza maswali kama hayo na kupata picha kamili? Hebu fungua fahamu zako na akili yako sasa.


Ndugu yangu Mkosefu, tambua kuwa, Mariamu sio kimbilio lako wewe mkosefu bali ni Yesu Kristo, Mungu Mwenye kuhimidiwa milele, ambaye alisema maneno haya kwa wakosefu wote…

Isaya 1:18 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. DHAMBI ZENU ZIJAPOKUWA NYEKUNDU SANA, ZITAKUWA NYEUPE KAMA THELUJI; ZIJAPOKUWA NYEKUNDU KAMA BENDERA, ZITAKUWA KAMA SUFU.  

Na tena alisema…

Matayo 11:28 NJONI KWANGU, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 

Huyo ndiye kimbilio la kweli na la pekee kwa wakosefu wote duniani, ukihubiriwa mwengine yoyote tofauti na huyo tambua kwamba unahubiriwa uongo, hivyo, dhehebu lolote lile likiwemo katoliki, linalofundisha kuna kimbilio lingine la wakosefu tofauti na Bwana Yesu ni la uongo, ondoka huko mara moja kwa usalama wa nafsi yako, toka katika hilo kanisa lililojaa mapokeo na mafundisho potofu yasiyokufikisha katika uzima wa milele bali Jehanam, toka katika hilo kanisa linalofundisha kuwaomba watu waliokufa mambo ambayo ni machukizo kwa Bwana (Kumb 18:11-12), ondoka katika hilo dhehebu linalokufundisha ukifa katika dhambi unaenda sehemu ya mateso kidogo (Toharani), kisha unaingia mbinguni, hayo ni mafundisho ya uongo ndugu usidanganyike, baada ya kifo hukumu ya Mungu juu ya roho yako ndiyo inayofuata (Waebrania 9:27), 

Toka katika hilo dhehebu kwani ndilo mwanamke (kanisa), mwenye jina lililoandikwa kwa siri “mama wa makahaba na machukizo ya nchi” (ufunuo 17:4-6), ambaye ni mji ule mkubwa wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi (Vatcan)..

Ufunuo 17:18 Na yule mwanamke uliyemwona, ni mji ule mkubwa, wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi. 


Kumbuka: Tunaishi katika siku ambazo Mwana wa Adamu yupo mlangoni kurudi, hivyo tengeneza mambo ya nyumba yako sasa kwa kutubu dhambi zako na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi na kudumu katika fundisho la mitume. 

Hizi ni siku za mwisho, usikubali kupotezwa na makanisa na mafundisho ya uongo;

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 03)


MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 02)


MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 01)


Mkia wa joka kubwa jekundu anaoutumia kuziangusha nyota chini ni nini? (Ufunuo 12:4)


UFALME WA MUNGU NI NINI, ULITOKA WAPI NA ULIANZA LINI?(sehemu ya 01)


Je! Kuna Mungu wawili? (Kulingana na Yohana 1:1)

LEAVE A COMMENT