MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 03)

Siku za Mwisho, Uncategorized No Comments

Shalom, nakukaribisha kwa mara nyingine tena katika mwendelezo wa makala hii fupi inayoangazia makanisa na mafundisho ya uongo yanayopotosha watu wengi nyakati hizi za mwisho, tulishatazama mawili huko nyuma katika sehemu ya kwanza na ya pili, endapo ulipitwa na sehemu hizo na unahitaji kuzipata, basi, unaweza tuandikia ujumbe kwa namba +255755251999 au +255625574252  ili uweze kutumiwa sehemu hizo.

Hii ni sehemu ya tatu (03) ya makala yetu, karibu.


WAADVENTISTI WASABATO


Ndugu mpendwa, unatakiwa kufahamu kuwa, Bwana Wetu Yesu Kristo hakuja kuanzisha dhehebu lo lote la dini hapa duniani, bali alikuja kuleta IMANI MOJA TU YA THAMANI KWA AJILI YA UKOMBOZI WA ROHO ZA WANADAMU, ndivyo biblia inavyosema katika….

2 Petro 1:1 Simoni Petro, mtumwa na mtume wa Yesu Kristo, kwa wale WALIOPATA IMANI MOJA NA SISI, YENYE THAMANI, KATIKA HALI YA MUNGU WETU, na Mwokozi Yesu Kristo. 

Ikimaanisha kwamba, ipo imani moja tu ya thamani katika Yesu Kristo, ile Imani iliyokuwepo katika makanisa ya kwanza kama ya Efeso, Korintho, Samaria, Yerusalemu, Galatia, Antiokia n.k, ndiyo imani hiyo hiyo inayotakiwa kuwepo pia katika kanisa lolote lile la kweli hivi sasa, hivyo, ukiona dhehebu lolote au Kanisa lo lote lile lenye mafundisho tofauti na hayo yaliyokuwapo katika makanisa ya kwanza, basi tambua kuwa, hilo kanisa ni la uongo, haijalishi linawafuasi wengi kiasi gani, au ni zuri kiasi gani au ni kubwa kiasi gani, unapaswa utoke huko kwa usalana wa roho yako, na moja wapo ya makanisa hayo ni hili la WAAVENTISTI WASABATO ambalo linaonekana Kama ni takatifu lakini limejaa mafundisho mengi potofu kutoka kwa ibilisi yaliyo kinyume na maandiko matakatifu.

Dhehebu hilo linafundisha watu kujiepusha na vyakula fulani kwa kisingizio kuwa, Mungu aliviita najisi (Walawi 11). 

Kwa kukosa ufunuo wa maandiko wamejikuta wakifarakana na Imani na kufuata mafundisho hayo ya mashetani yanayowazuia watu wajiepushe na vyakula fulani (1 Timotheo 4:1-3) na kuufundisha uongo huo kwa watu na kuwapoteza mbali kabisa na imani ya kweli, ndugu kuwa makini.

Bwana Yesu alisema, maneno yake na mafundisho yake sio yake yeye bali ni yake yeye aliyempeleka (Yohana 7:16), na tena maandiko yanasema..

Marko 7:18 Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi;

19 kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? KWA KUSEMA HIVI ALITAKASA VYAKULA VYOTE.   

Sasa, ikiwa kwa neno hilo la Bwana ambalo ni la Mungu vyakula vyote vilitakaswa, hayo mafundisho mengine ya kusema vyakula fulani ni najisi yametoka wapi kama si kwa ibilisi? Na tena bila inasema katika..

1 Wakorinto 10:25 Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri; 

Na tena inasema katika 

Waebrania 13:9 Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo hawakupata faida. 

Kanisa linalofundisha watu wajiupushe na vyakula fulani kwa sababu ni najisi ni la uongo toka katika hilo kanisa. Watu wanaofundisha neema ya wokovu haitarudi tena katika taifa la Israeli sio kanisa la Mungu kwani lipo kinyume na andiko linalosema..

Warumi 11:25 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.

26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao. 

Kanisa linalofundisha kuwa muhuri wa Mungu ni siku ya sabato ni la uongo biblia haijasema hivyo, muhuri wa Mungu ni Roho Mtakatifu (Waefeso 1:13). Kanisa lanalofundisha Yesu Kristo aliingia katika hekalu la mbinguni mwaka 1844 ni la uongo na la mafundisho potofu kabisa ambayo hayapo katika biblia, kanisa linalofundisha majuma 70 ya Danieli yamekwisha timia ni la uongo kwani biblia inasema bado hayaja timia. Kanisa linalofundisha mtu akifa hakuna kinachoendelea ni la uongo biblia haitufundishi hivyo, ni ama roho yako inapokelewa na Yesu Kristo (Wafilipi 1:23, Matendo 7:59), ama ipokelewe na mapepo kuzimu kwenye mateso.


Kumbuka: sio kila anayemuhubiri Kristo anamuhubiri kwa lengo la wewe kuufahamu ukweli ili uurithi uzima wa milele, wengine wanamuhubiri Kristo kwa lengo la kubishana (fitna na husuda), wengine kwa lengo la kujipatia faida, wengine kwa lengo la kutetea mashirika yao, taasisi zao, na madhehebu yao kwa kuwa wanajipatia huko vyeo, wadhifa, umaarufu na fedha, na wengine wanamuhubiri Kristo kwa upendo ili kukuponya nafsi yako na moto wa milele, hivyo kuwa makini.

Wafilipi 1:15 Wengine wanahubiri habari za Kristo kwa sababu ya husuda na fitina; na wengine kwa nia njema. 

Hizi ni siku za mwisho, usikubali kupotezwa na makanisa na mafundisho ya uongo;

Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.


Mada zinginezo:

Je! Tunapaswa kushika sabato kulingana na Isaya 66:23?


Sabato zilizowekwa na wanadamu ni zipi? 

Je! Ni kweli Bwana Yesu alishika sabato kuninganana luka 4:16?


Je! Ni kweli majuma sabini aliyoambiwa Daniel yamekwisha timia?(Daniel 9:23-27)


MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 02)


MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 01)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *