Ni Mungu gani tutakayemwona na kufanana nae atakapodhihirishwa? (1 Yohana 3:2)

Mungu, Uncategorized No Comments

Swali: Biblia inasema katika [1 Yohana 3:2]

1 Yohana 3:2 Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa ATAKAPODHIHIRISHWA, TUTAFANANA NAYE; kwa maana TUTAMWONA kama alivyo. 

Je! Ni Mungu gani huyo ambaye atakapodhihirishwa tutamwona na kufanana naye? Je! Ni Mungu Baba? Mwana? au Roho?


Jibu: Mungu anayezungumziwa hapo ni MMOJA TU, YESU KRISTO, ambaye ni

  1. Baba, na tena sio Baba tu ila ni wa milele (Isaya 9:6), 
  2. tena ni Mwana (Mathayo 14:33), 
  3. na pia ni Roho (2 Wakorintho 3:17)

Wala hakuna Mungu watatu, hivyo ni vyeo tu kama vile sehemu nyingine anavyofahamika kwa jina la Adamu wa pili, au mwana wa Adamu au Mwana-kondoo, au mwana wa Ibrahimu, au Mwana wa Daudi, au Mzee wa siku, au alipochukua nafasi ya Musa kama kiunganishi kati ya Mungu na Waisraeli (wa kimwili na kiroho), na vyeo vingine vingi sana ambavyo hatuwezi vimaliza hapa, ila ni huyo huyo Mungu mmoja tu, aliye wanunua watu wa kanisa lake kwa damu yake mwenyewe.

Matendo 20:28 Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha KANISA LAKE MUNGU, ALILOLINUNUA KWA DAMU YAKE MWENYEWE.  

Sasa, ili tuelewe kuwa Mungu anayezungumziwa hapo ni Yesu Kristo, tuzingatie maneno haya katika waraka wa Yohana 

1 Yohana 3:2 Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa ATAKAPODHIHIRISHWA, TUTAFANANA NAYE; kwa maana TUTAMWONA kama alivyo. 

  1. ATAKAPODHIHIRISHWA (yaani Mungu)
  2. TUTAFANANA NAYE 

Harafu tusome kifungu kifuatacho katika waraka wa mtume Paulo ”zingatia maneno yaliyoandikwa kwa herufi kubwa”

Wakolosai 3:4 KRISTO ATAKAPOFUNIWA, aliye uhai wetu, NDIPO NA NINYI MTAFUNULIWA PAMOJA NAYE KATIKA UTUKUFU.

Hapo anaposema “Kristo atakapofunuliwa (yaani Mungu atakapodhihirishwa)” ndipo na sisi tutakapofunuliwa pamoja naye (yaani kufanana naye katika Utukufu), Kwa sababu imeandikwa wenye haki watangaa kama jua katika ufalme wa Baba yao, kumaanisha Utukufu ule ujao (Mathayo 13:43), umeona hapo?.. Hivyo, Yesu Kristo ndiye Mungu pekee, Mwenye kuhumidiwa milele, wala hakuna kama yeye, sifa na utukufu ni vyake milele na milele, Amina.

Warumi 9:4 ambao ni Waisraeli, wenye kule kufanywa wana, na ule utukufu, na maagano, na kupewa torati, na ibada ya Mungu, na ahadi zake; 

5 ambao mababu ni wao, na katika hao ALITOKA KRISTO KWA JINSI YA MWILI. NDIYE ALIYE JUU YA MAMBO YOTE, MUNGU, MWENYE KUHIMIDIWA MILELE. AMINA.

Siri ya utauwa (uungu) ni kuu mno.


Mada zinginezo:

UMEMWAMINI YESU KRISTO KWA NAMNA GANI?


INJILI YA KRISTO HAIENDI NA WAKATI


Mkia wa joka kubwa jekundu anaoutumia kuziangusha nyota chini ni nini? (Ufunuo 12:4)


NAO WATAJIEPUSHA WASISIKIE YALIYO KWELI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *