Neno Mataifa lina maana gani Katika biblia?

Uncategorized No Comments

JIBU…

Mpango wa Mungu wa kurejesha uhusiano wake na mwanadamu ulianza na taifa moja tu, Israeli ambalo liliundwa na Ibrahimu na Isaka. Jumuiya ya Waisraeli ilikua ni kuwa jeshi kubwa la makabila 12, na watu wa mataifa walikuwa watu wa jamii nyingine. Mungu amekuwa akitembea na Israeli pekee kwa zaidi ya miaka 1,500, bila kushughulika na mataifa yote.

Mungu alikuwa na mpango mkubwa kwa Mataifa, lakini mtoto wa pili hawezi kuzaliwa kabla ya wa kwanza. Taifa la Israeli ni mzaliwa wa kwanza wa Mungu, na watu wa mataifa ni wazaliwa wa pili.

Kutoka 4: 22 “Nawe umwambie Farao, Bwana asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu;

23 nami nimekuambia, Mpe mwanangu ruhusa aende, ili apate kunitumikia, nawe umekataa kumpa ruhusa aende; angalia basi, mimi nitamwua mwanao, mzaliwa wa kwanza wako”.

Mungu alianza mpango wake kwa kumleta Mwana wake mpendwa Yesu Kristo kuwa sababu ya wokovu kwa watu wote wa mataifa.

Tangu wakati wa Bwana Yesu hadi sasa, watu wa mataifa yote wanaweza kumkaribia Mungu na kurithi baraka za kiroho sawa na walizopewa Israeli. Hii ndiyo siri ya Mungu, ambayo ilifichwa kwa miaka mingi.

Warumi 11:25 “ Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili”.

Paulo, Mwisraeli, aliandika siri kwa ufunuo wa Roho, akisema kwamba mataifa ni warithi wa urithi mmoja na mwili, na washiriki katika ahadi ya Mungu kwa njia ya injili.

Waefeso 3:4 “Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo.

5 Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho;

6 YA KWAMBA MATAIFA NI WARITHI PAMOJA NASI WA URITHI MMOJA, NA WA MWILI MMOJA, NA WASHIRIKI PAMOJA NASI WA AHADI YAKE ILIYO KATIKA KRISTO YESU KWA NJIA YA INJILI”.

Lakini lipo jambo la kuzingatia kwa watu wa mataifa maana,
Baada ya Bwana Yesu kuondoka duniani, zaidi ya miaka 2,000 imepita, kipindi cha neema kwa Mataifa kitaisha na kufikia kilele katika unyakuo. Baada ya Unyakuo, Mungu atarudi kwa Israeli kwa kipindi kifupi cha juma moja(miaka saba), na hukumu ya mataifa kisha, utaanza utawala wa amani wa Yesu Kristo kwa miaka elfu moja.

Kwasasa rohoni mtu yeyote ambaye yupo nje ya Kristo anajulikana kama Mataifa.
Hivyo ikiwa bado ujaokoka, ujamkiri Yesu Kristi katika maisha yako, wakati ni huu usisubiri kesho Neema ya ambayo imekuja kwa kwetu sisi wamataifa haitadumu, ikiwa leo umesikia injili usishupaze shigo yako
Mwamini Yesu nawe utaokoka na dhiki kuu

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Maran atha.
Kwa msaada wa wokovu wasiliana nasi kwa namba hizi: +255693036618 au +255789001312.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *