Matowashi ni watu gani?

Uncategorized No Comments

JIBU….

Matowashi ni watu waliojitoa wakfu kwa ajili ya Mungu (ufalme wa mbinguni) , ambao hawajihusishi na mambo ya wanawake yaani kuwa na mke au familia…
Mfano wa matowashi katika biblia
Mtume Paulo, Yohana mbatizaji, Barnaba, Eliya Mtishbi na Bwana wetu YESU KRISTO

Lakini kuna jambo ambalo Bwana Yesu alilisema katika kitabu cha Mathayo, ambalo lilikanusha kuhusu matowashi

Tusome

Mathayo 19:10-12
[10]Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.

[11]Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.

[12]Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.

Hapo Bwana alielezea Aina za matoashi namna walivyogawanyika

Aina za Matowashi

1 Matowashi waliozaliwa na hali hiyo
Hawa ni wale watu ambao toka wapo tumboni mwa mama zao Mungu aliwafanya kuwa matowashi

2 Matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi
Hawa ni watu ambao wamefanywa na watu yaani wamehasiwa kwa ajili ya ufalme wa Mbinguni.

3 Matowashi waliojifanya matowashi
Hili ni kundi ambalo lenyewe limeamua kuwa hivyo, pasipo kufanywa na watu, wala hawakuzaliwa hivyo, ila wameamua kuwa hivyo kwa kutojihusisha na mambo ya ndoa, yaani wanaamua kujihusisha na mambo ya Ufalme wa Mbinguni tu
Mfano mtume Paulo nk…

Lakini jambo hili si lazima kulifanya kama mtu atakuwa hajazaliwa katika hali ya utowashi, ndiyo maana Bwana Yesu alisema mtu yoyote awezaye kulipokea neno hilo na alipokee
Kama mtu hataweza basi hakuna tatizo na asilipokee lakini si lazima
Maana jambo hili mtu ajilazimishi wala hatumii nguvu kabisa kuwa hivyo bali ni kitu kinachotoka moyoni , anakuwa anaona ni bora awe karibu na Mungu kuliko kuwa na ndoa…

Na hii si kwa wanaume tu hata kwa wanawake,
Mwanamke pia aliyeamua kutokujihusisha na mambo ya mme na akataka kujihusisha na kumtafuta Mungu tu naye pia ni towashi.

Lakini paulo naye alisema hili kwa nguvu ya Roho Mtakatifu alitoa ushauri

1 Wakorintho 7:25-26
[25]Kwa habari za wanawali sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kwa rehema za Bwana kuwa mwaminifu.

[26]Basi, naona hili kuwa jema, kwa ajili ya shida iliyopo, kwamba ni vema mtu akae kama alivyo.

Hivyo jambo hili ukiweza kulipokea ni vyema, na usipoweza pia si vibaya, zaidi tudumu katika kuyatenda mapenzi ya Mungu, kwa
Kuutafuta ufalme na haki yake kwa bidii kabisa

Ubarikiwe

Je!, umeokoka, kama bado bado nafasi unayo mpe leo Kristo maisha yako akutue mizigo Yote ya dhambi, akusamehe na kukupa uzima wa Milele..

Bwana Yesu akubariki sana.

Tafadhali washirikishe na wengine ujumbe huu wasiliana nasi.

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312.

Kwa Ushauri/Maombezi/Maswali
Wasiliana nasi kwa namba hizi
+225693036618/ +255789001312

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *