SIFONGO NA SIKI NI NINI?

Uncategorized No Comments

JIBU: Tusome..

Yohana 19: 28  “Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.

29  Kulikuwako huko chombo kimejaa siki; basi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakampelekea kinywani.

30  Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake”

Sifongo ni kiswahili cha neno la kingereza Sponge ambalo tumezoea kulitaja neno hilo kama SPONCHI au SPONJI… Na yapo masponchi ya aina nyingi, yaliyozoeleka sana na wengi ni yale yaliyotengenezwa kwa malighafi ya godoro, Matumizi yake yanakuwa kwa kuoshea vyombo na matumizi mengine, kwasababu yanakuwa yanauwezo wa kufyoza maji na kutengeneza povu. Enzi za zamani (za Bwana Yesu) yalikuwepo pia masponji, ambayo yalikuwa yanakaribiana sana kufanana na haya ya kwetu ya sasa…

Hivyo Sifongo ni sponji. Sasa tukirudi kwenye maandiko tunasoma yule askari, alitwaa hiyo Sifongo na kulitia kwenye SIKI, na lengo la kufanya hivyo ni ili hiyo SIKI ijifyonze kwenye hiyo sifongo.

SASA SIKI NI NINI?

Siki ni kiungo ambacho kinakuwa katika kimiminika, kinachotengenezwa kwa kuchachushwa kama vile zinavyotengenezwa pombe…Na kimiminika hicho kazi yake ni kuongeza ladha kwenye chakula au kukihifadhi chakula kisiharibike…

Zipo siki za aina nyingi kulingana na jamii za watu na tamaduni. Huku kwetu Afrika hususani Afrika mashariki, Siki haziwi katika mfumo wa kimiminika kizito sana…lakini nchi nyingine zinatengenezwa viwandani na kuwa kama Maji (mfano wa hizo ni zile vanilla zinazotumika kwenye ice-cream na keki ambazo zinakuwa zinahifadhiwa kwenye kachupa kadogo), na pia maeneo ya Mashariki ya kati, ikiwemo Taifa la Israeli, siki zao zilitengenezwa na Zabibu, hivyo zilikuwa hazina tofauti sana na Divai.Kwahiyo siki iliyotumika pale msalabani ilikuwa ni kama Divai, lakini si divai kabisa…Na zilitumika katika matumizi ya vyakula. Hivyo wale askari walichovya sifongo kwenye siki na kuiweka kwenye mti, ili ifike juu pale msalabani alipokuwepo Bwana Yesu.(kwasababu siki kwaasili ni INA UKALI, inaukakasi na ni chungu na ina tindikali nyingi, kwa ufupi haifai kuwekwa katika kinywa cha mwanadamu kwa ukali wake, walifanya vile ili Mwili wa Bwana Yesu ukaukiwe maji…kwasababu walimsikia akisema Naona kiu.

Sasa ipo siri kubwa sana katika tukio hilo lililotendeka hapo juu msalabani, Kama utapenda kufahamu zaidi siri hiyo basi endelea kutufatilia kwa Mafundisho tunayotuma kila wakati…

Bwana akubariki.

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *