Swali: kuna injili ngapi katika biblia na injili ipi ni ya kweli?
Jibu: Kuna makundi mawili tu ya injili katika maandiko. Kundi la kwanza ni Injili ya Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo ambayo inaleta wokovu wa roho za watu na kundi la pili ni injili zote ambazo hazileti wokovu wa roho zetu.
Maandiko yanathibitisha kuwa kuna ijili nyingine tofauti na ile ya kwanza yaani injili ya Kristo
2 Wakorinto 11:4 Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye!
Hivyo basi, kuna injili moja inayoleta wokovu wa roho zetu ambayo ni ya Bwana Yesu, injili ya Kristo na maisha yake ina waandishi wanne wa vitabu vya injili katika biblia ambao ni
Mathayo
Marko
Luka na
Yohana
Na injili hii ilianza kuhubiriwa tangu zamani na Mungu mwenyewe pale alipomwambia Ibrahimu kuwa, kupitia mzao wako kila kabila la ulimwengu huu litabalikiwa akimaanisha kuwa baraka hiyo ni Yesu Kristo.
Wagalatia 3:16 Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazao, kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo.
17 Nisemalo ni hili; agano lililothibitishwa kwanza na Mungu, torati iliyotokea miaka mia nne na thelathini baadaye hailitangui, hata kuibatilisha ile ahadi.
Na pia injili hii ya Kristo ilihubiriwa na mitume kama Filipo, Petro, Yohana, n.k na pia inaendelea kuhubiriwa hadi sasa na watumishi wa Mungu wa kweli kama tulivyoipokea pasipo kuchanyanya na uongo wowote
2 Wakorinto 4:2 lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu.
Lakini vivyo hivyo pia, na hizo injili nyingine zenye lengo la kuwapoteza wanadamu. Kama zilivyohubiriwa na mafarisayo na watu ambao waliokuwa wakiwashurutisha watu washike siku n.k na zenyewe zinahubiriwa hata sasa.
Hivyo basi kwa kuhitimisha ni kwamba, kuna injili za aina mbili, ya kwanza ni ya Bwana Yesu iliyoandikwa na waandishi wanne na kuhubiriwa na mitume zamani na hadi sasa inahubiriwa na watumishi wa Mungu wa kweli. Na ya pili ni injili zote ambazo zipo kinyume na injili ya Kristo.
Je! Umeshampa Bwana maisha yako na kuitii injili yake? Basi mlango wa neema bado upo wazi hivyo tubu leo kwa kumaanisha na kumpa Bwana maisha yako na kisha kubatizwa katika ubatizo sahihi.
Bwana akubariki. Shalom
Mada zinginezo:
Kusaga meno, ni nini kama inavyozungumziwa katika maandiko?
Kuuza cheni na hereni ni sawa kwa Mkristo?
Je! matumizi ya mimea ya asili kwa matibabu ni dhambi kwa mkristo?