Je! Bikira Maria ni mkamilishaji wa mahitaji yetu pale tunapokwama? (kulingana na Yohana 2:3-5)

SWALI: Je! Bikira Maria ni mkamilishaji wa mahitaji yetu pale tunapokuwa na shida mbali mbali kwa kutuombea kwa mwanawe Bwana Yesu? Kwasababu tunaona ule wakati wa harusi huko kana, mji wa Galilaya, wale watu walipopungukiwa na divai, Mariamu alimfuata Bwana Yesu na kumweleza shida yao na baada ya hapo, Bwana akakamililisha hitaji lao la divai.

Yohana 2:3 Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai. 

4 Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia.

 5 Mamaye akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambia, fanyeni. 

JIBU: Bikira Mariamu si mkamilishaji wa mahitaji yetu hata kidogo kwa kutuombea kwa Bwana Yesu. Na si yeye tu, bali hata watakatifu wengine wote waliopita kama Ibrahimu, Musa, Eliya, Yohana, Samweli, Daudi n.k kwasababu kwa kufanya hivyo tutakuwa tunawaomba wafu, na maandiko matamatifu yanasema kuwa, yoyote anayewaomba wafu anafanya MACHUKIZO mbele za Mungu.

Kumbukumbu La Torati 18:10  Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 

11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, WALA MTU AWAOMBAYE  WAFU

12 KWA  MAANA MTU ATENDAYE HAYO NI CHUKIZO KWA BWANA; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako. 

Viongozi wengi vipofu wa dini  sasa hivi, wanawafungia watu ufalme wa Mungu kwa kuwafanya watu waende kinyume na Mungu kwa kuwafundisha watu kuwaomba hao watu waliokufa, na mafundisho mengine mengi ambayo msingi wake si biblia takatifu bali mapokeo, ndugu yangu tambua kuwa hao wapo chini ya laana kwasababu hakuna mtume hata mmoja kwenye maandiko aliyewafunsisha watu kuwa wanapaswa kumwomba Mariamu

Wagalatia 1:8  Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. 

Kinyume chake, Mariamu na yeye alikuwa ni miongoni mwa washirika wa kanisa la mitume pale Yerusalumu na siku ya pentekoste alipokea Roho mtakatifu yeye pamoja na watoto zake.

Matendo Ya Mitume 1:13 Hata walipoingia, wakapanda orofani, walipokuwa wakikaa; Petro, na Yohana, na Yakobo, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo wa Alfayo, na Simoni Zelote, na Yuda wa Yakobo. 

14 Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, PAMOJA NAO WANAWAKE, NA MARIAMU MAMA YAKE YESU, NA NDUGU ZAKE. 

Na ndio hawa ambao walipokea Roho Mtakatifu ile sikukuu ya pentekoste na Mariamu akiwepo pale 

Matendo Ya Mitume 2:1 Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.

 2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. 

3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. 

Turudi kwenye swali letu.

Kama ukitumia mfano huo wa harusi ya huko kana kuhalalisha kuwa Mariamu ni  mkamilishaji wa shida zetu kwasababu aliwaombea watu wale kwa Bwana Yesu, na Bwana akatenda jambo pale, basi hatuna budi pia kusema kuwa, hata wale wazee wa kiyahudi pia ni wakamilishaji wa shida zetu na tunapaswa kuwaomba ili watufikishie maombi yetu kwa Bwana, kwani hata wao pia walimuombea yule akida wa Kirumi kwa Bwana na yule akida alipokea alichokipata kwa imani kama wale watu wa kana walivyopokea pia. 

Luka 7:3  Aliposikia habari za Yesu, alituma wazee wa Wayahudi kwake kumwomba aje amponye mtumwa wake.

 4 Nao walipofika kwa Yesu, walimsihi sana wakisema, Amestahili huyu umtendee neno hili; 

Umeona? Alichokifanya Marimu ndicho walichokifanya hao wazee wa kiyahudi.

Lakini pia, hata kwa wakristo wa zamani waliotutangulia mfano Paulo na wenzake. Kuna kipindi walipitia dhiki huko Asia hadi wakakata tamaa ya kuishi, lakini katika dhiki yao hawakumtumainia Mariamu pale, wala nabii Eliya, wala nabii Musa. Bali kinyume chake walimtumainia Mungu pekee ambaye aliwaokoa na ambaye atazidi kutuokoa

2 Wakorinto 1:8  Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi.

 9 Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu ili tusijitumainie nafsi zetu, bali tumtumaini Mungu, awafufuaye wafu, 

10 aliyetuokoa sisi katika mauti kuu namna ile; tena atatuokoa; ambaye tumemtumaini kwamba atazidi kutuokoa; 

Hivyo, hatupaswi kumwomba Mariamu, hao wazee wa kiyahudi, wala mtu yoyote yule.

Tafadhari, washirikishe na wengine habari hii njema.

Bwana akubariki, Shalom.


MADA ZINGINEZO

Je! Ni dhambi kibiblia kuwaomba wafu (watakatifu)?


Biblia imeruhusu ubatizo wa vichanga (kulingana na matendo 16:33?)


Pazia la Hekalu ni nini katika biblia?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *