Je! matumizi ya mimea ya asili kwa matibabu ni dhambi kwa mkristo?

SWALI: Matumizi ya mimea ya asili kama vile tangawizi, alovera, mizizi ya mwarobaini, vitunguu swaumu, magome ya miti, majani ya msonobari n.k kwa lengo la matibabu ni dhambi kwa mkristo? 

JIBU: matumizi ya mimea kama hiyo kwa kwa lengo la tiba si dhambi. Kama unaumwa tumbo na unafahamu kuwa majani ya mpera ni dawa, basi, unaweza chemsha ukanywa, kama una kikohozi na unajua tangawizi ni dawa, basi, unaweza chemsha ukanywa, kama unaumwa na kichwa na unafahamu mizizi ya mti fulani ni dawa, basi, unaweza chemsha ukanywa, wala si dhambi mbele za Mungu, kwani hata Mungu wakati anaviumba alisema tuvitumie pia kama chakula.

Mwanzo 1:29  Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu; 

30 na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo. 

Lakini endapo ukavihusisha vitu hivyo na masuala ya uganga, uchawi na ushirikina, matambiko na mizimu, basi inakua ni dhambi mbele za Mungu na tena ni machukizo makubwa sana, kwani hizo ni ibada za miungu mingine ambazo zinamtia Bwana wivu sana. Hivyo mkristo yoyote akihusisha mizizi fulani au majani fulani na uganga au mizimu au uchawi hiyo inakua ni dhambi mbele za Mungu.

Ni kama vile tu, tunavyotumia leo hii nazi kwenye mapishi, mayai, kuku tembe, jogoo, unga n.k kwa lengo la kujipatia chakula, si dhambi mbele za Mungu, lakini kama vikitumika kwa lengo la uganga, kuroga, kupiga bao, matambiko n.k basi,  hapo ni dhambi mbele za Mungu.

Je! Umeshampa Bwana maisha yako na kubatizwa katika ubatizo sahihi? kama bado unangoja nini ndugu yangu? Mlango wa neema bado upo wazi, fanya hima ndugu kabla hujafungwa.

Luka 13:25  Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako; 

26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.

 27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu. 

28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje. 

Ndugu yangu, hayo maneno aliyasema Bwana Yesu mwenyewe na lazima yaje kutimia kama yanyotimia sasa hivi mambo aliyoyasema ya tauni na vita. Hivyo amua leo kumpokea Bwana Yesu maishani mwako.

Bwana akubariki. Shalom.


Mada zinginezo:

Je! kupiga punyeto ni dhambi kwa mujibu wa biblia?


Je! Ni kweli Bwana Yesu alishika sabato kuninganana luka 4:16?


Ni lini Bwana alivitakasa vyakula vyote kulingana na 1 Timotheo 4:3?


Kwanini watu wa Kanisa la kwanza walionekana kujazwa Roho Mtakatifu zaidi ya Mara moja?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *