Marago ni makazi ya muda ambayo hutumiwa kwa madhumuni maalumu, kama vile wakati wa vita, watu waliweka kambi au mahema katika maeneo mbalimbali, hayo ndiyo marago
Kwa mfano ukisoma Waamuzi 10:17-18 inasema..
[17]Wakati huo wana wa Amoni walikutana pamoja, wakapanga marago huko Gileadi. Wana wa Israeli nao wakajikusanya wakapanga marago Mispa.
[18]Na hao watu, wakuu wa Gileadi, wakaambiana wao kwa wao, Je! Ni mtu yupi atakayeanza kupigana na wana wa Amoni? Yeye atakuwa ni kichwa juu ya wenyeji wote wa Gileadi.
Wana wa Israeli waliweka kambi za kijeshi huko Mispa, wakati walipokuwa katika safari yao ya kuelekea nchi ya ahadi, walishi kwa muda maeneo Kadha wa kadha.
Kwa Mfano ukisoma tena; Kutoka 29:13-14
[13]Kisha twaa mafuta yote yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo juu yake, uyateketeze yote juu ya madhabahu.
[14]Lakini nyama yake huyo ng’ombe, na ngozi yake, na mavi yake, utayachoma kwa moto nje ya marago; ni sadaka kwa ajili ya dhambi.
Akiwa na maana hivyo viungo vya ndani watavichoma mbali na pale wana wa Israeli walipoweka makambi..
Neno hilo italisoma pia katika vifungu hivi;
Kutoka 36:6, Walawi 4:21, 10:5, Waamuzi 21:12.
Ibrahimu, licha ya utajiri wake, aliamini kusudi la milele la kuishi katika mbingu na dunia mpya, licha ya kuitwa Baba wa imani. Aliishi kama mpita njia katika ulimwengu huu, akitambua uwepo wetu wa muda.
Waebrania 11:9-10
[9]Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.
[10]Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu….
[14]Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe.
[15]Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea.
[16]Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.
Je! Na wewe umejikita au umeweka marago yako kwa muda hapa duniani?. Ndugu ishi kama mpitaji, kwa kutokuruhusu mawazo yako kumezwa na tamaa za huu ulimwengu. Kuwa na kiasi, mtafute muumba wako angali muda upo. Okoka leo Yesu akupe msamaha wa dhambi, ikiwa upo tayari kumpokea Kristo basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Bwana akubariki.
Kwa mawasiliano zaidi +255693036618/+255789001312
Jiunge pia na Channel yetu ya WhatsApp.
“ NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Masomo mengine:
Utajiri huongeza rafiki wengi; Bali maskini hutengwa na rafiki yake