Mkia wa joka kubwa jekundu anaoutumia kuziangusha nyota chini ni nini? (Ufunuo 12:4)

SWALI: Bwana Yesu apewe sifa, naomba kuuliza swali hili, je! Mkia wa joka kubwa jekundu ambao anautumia kuziangusha nyota za mbinguni chini ni nini?

Ufunuo 12:3  Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.

 4 NA MKIA WAKE WAKOKOTA THELUTHI YA NYOTA ZA MBINGUNI, NA KUZIANGUSHA KATIKA NCHI. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake. 

JIBU: Kumbuka hayo  aliyoyaona mtume Yohana akiwa katika kisiwa cha Patmo ni maono ambayo yanafunua au kuwakilisha kitu fulani, kwa mfano tukisoma kitabu hicho hicho cha ufunuo sura ya 13 biblia inasema..

Ufunuo 13:1  Kisha nikaona MNYAMA akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.

 2 Na yule MNYAMA niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. 

Sasa hapo biblia haimaanishi kuwa atatokea mnyama kama huyo mwenye umbo kama la chui, miguu ya dubu, kinywa cha simba n.k hapana! (Sidhani kama Mungu ameumba kiumbe kama hicho duniani), Hiyo ni kufunua na kuwakilisha sifa fulani fulani tu! lakini anayezungumziwa hapo ni MTU (ambaye atapewa nguvu na joka yaani shetani ili kuidanganya dunia), na mtume Paulo alishalihubiri hilo katika kanisa la Kristo siku nyingi tu..

2 Wathesalonike 2:3  Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa YULE MTU wa kuasi, MWANA WA UHARIBIFU

Umeona hapo kuwa mnyama aliyetoka baharini ni MTU kama mtume Paulo alivyohubiri na si mnyama harisi? Lakini hata Bwana Yesu pia alinena habari zake kuhusu huyo mtu (soma Yohana 5:43), hivyo basi, biblia iliposema, huyo joka yaani shetani, kuwa anatumia MKIA WAKE kukokota nyota za mbinguni na kuziangusha chini, haina maana kwamba, ibilisi anao mkia mrefu kama wa kenge au mjusi au mamba unaofika hadi juu na kuutumia huo kudondosha nyota chini hapana! Maana yake sio hiyo, ila inamaanisha kuwa, ibilisi anatumia MANABII WA UONGO kuwapotosha watu wa Mungu kwa sababu mkia ni Manabii wafundishao uongo..

Isaya 9:15  Mzee mwenye kuheshimiwa ndiye kichwa, NA NABII AFUNDISHAYE UONGO NDIYE MKIA. 

Hivyo, mkia ambao ibilisi anaoutumia kuwaangusha chini binadamu (nyota) kutoka upande sahihi wa Mungu (mbinguni) ni MANABII WAFUNDISHAO UONGO na sio mkia harisi kama wa mjusi au kenge. Lakini pia, biblia inaposema manabii wafundishao uongo inamaanisha mitume, wainjilisti, maaskofu, wachungaji na waalimu wote wasiofundisha injili ya kweli ya msalaba ya Bwana Wetu Yesu Kristo, hivyo ukijiona upo chini ya dini na madhehebu yanayofundisha injili nyingine kabisa, ambayo haipo kwenye biblia kama vile ubatizo wa vichanga, wanawake kuwa wachungaji na maaskofu, kuwaomba marehemu, kufundishwa kunena kwa lugha na mtu falani, maji, chumvi, na keki za upako, kuvaa vimini na suruali kwa wanawake kanisani, kuhubiriwa mafanikio tu, mafanikio tu na huku hukemewi dhambi n.k, basi tambua kuwa, umeshaangushwa chini na mkia wa shetani kutoka katika njia ya kumfikia Mungu, hivyo inuka, toka huko na igeukie injili ya kwenye biblia yako takatifu iliyohubiriwa na mitume.

Bwana akubariki, shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

 +255652274252 / +255789001312


Mada zinginezo:

Je! Bwana Yesu alikuwa ni mdhambi kulingana na Mathayo 3:6? 

Ni lini Bwana alivitakasa vyakula vyote kulingana na 1 Timotheo 4:3?


Bado Bwana Yesu anasema nawe kwa mifano?


Kwanini watu wa Kanisa la kwanza walionekana kujazwa Roho Mtakatifu zaidi ya Mara moja?


Kupiga panda ni nini katika  (Mathayo 6:2)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *