WIBARI NI NANI?

Maswali ya Biblia No Comments

Wibari ni nani, na kwa nini wametajwa kama viumbe wanne wenye akili nyingi
(Mithali30:26)

Wibari ni wanyama wadogo ambao mwonekano wao, unakaribiana na sungura, wanajulikana pia kwa jina lingine kama pimbi, kwanga au perere

Na wanyama hao wametajwa sana katika maandiko mbalimbali
Mfano

Zaburi 104:18

[18]Milima mirefu ndiko waliko mbuzi wa mwitu,
Na magenge ni kimbilio la wibari.

Mambo ya Walawi 11:4
[4]Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.

Mithali 30:24-26

[24]Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo;
Lakini vina akili nyingi sana.

[25]Chungu ni watu wasio na nguvu;
Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari.

[26]Wibari ni watu dhaifu;
Lakini hujifanyia nyumba katika miamba.

Lakini kwanini maandiko yawataje kama moja ya wanyama wenye akili dunia japo ni dhaifu

Tabia na sifa ya wanyama hao kwanza hawali nyama, pili hawana mbio hawakimbii sana, kama wanyama wengine mfano chui, simba swala nk.. kwa ufupi wibari ni dhaifu sana

Japo wana udhaifu lakini, hutengeneza nyumba zao kwenye mapango ya miamba mirefu sana na migumu, ambayo hata adui zao hawawezi kwenda ili kuwadhuru, si rahisi hata kuwakamata kutokana na mahali walipojitengenezea nyumba zao .

Ukitofautisha na wanyama wengine ambao, wengine hujitengenezea nyumba zao kwa kuchimba machimo ardhini, wengine juu ya miti nk ukiangalia wanyama hawa wanaotengeneza nyumba zao kwa mfumo huo wa kuchimba mashimo huwa ni rahisi kushambuliwa na adui zao, au labda mvua ikinyesha au upepo ukivuma huwa ni rahisi nyumba zao kuharibika, hii ufanya hata maisha yao kuwa hatarini mda wote, tofauti na wibari ambao wao hata ije dhoruba, mvua upepo au maadui ni ngumu sana kupatwa na matatizo, japo wanaonekana ni dhaifu siyo machalili lakini ni viumbe vyenye akili Kubwa sana

Inafunua nini katika maisha yetu, kupitia wanyama hawa wibari

Lazima nasi tujitazame je usalama wetu au maisha tunayalinda kwa kujenga wapi, je kwenye mashimo, miti, miamba, ama vichunguu.
Hili ni jambo muhimu ambalo kila mwanadamu anapaswa alifahamu

Mathayo 7:24-27
[24]Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;

[25]mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.

[26]Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;

[27]mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.

Leo hii umelisikia neno la Mungu, umesikia Yesu pekee ndiye anayeokoa, Yesu pekee ndiye atupaye uzima wa milele, na bado umeshupaza shingo yako utaki kumkukubari hutaki awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako, unategemea nini, kukosa matatizo na mashambulizi ya ibilisi maishani mwako, hayo ni lazima yakupate kwa sababu nyumba yako umejenga mahali ambapo si salama ndiyo maana kila siku upo katika mashaka, wasiwasi na hofu za maisha, hofu za kurongwa nk..

Lakini ili kuondokana na hayo, Yesu yeye mwenyewe alisema
Kila atakaye sikia maneno yangu na kuyatii atafananishwa na mtu mwenye akili aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba ambaye hata pepo zikivuma hazita ipiga nyumba hiyo

Mwamba wa maisha yetu ni Yesu Kristo peke yake tofauto na hapo hakuna, sasa itakuwa ni ajabu leo hii Tushindwe akili na wanyama hawa wibari kwa kukosa utii

Mkaribishe leo Yesu Kristo maishani mwako ili uwe salama

Shalom.

Kwa maombezi/Ushauri/Maswali/Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba hizi

+225789001213/ +225693036618

Jiunge pia na Channel yetu ya  WhatsApp. 

“ NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Masomo mengine:

Kibanzi na Boriti kwenye biblia vinamaanisha nini?

Je kujichua/ kufanya punyeto (masturbation) ni dhambi?

Arabuni maana yake ni nini? ( Waefeso 1:14)<< KANISA NI NINI? na je linaundwa na nani?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *