Je! Ni sawa kuwa na sala au maombi maalum kwa Malaika fulani kibiblia?


SWALI: Je! Kuwa na sala au maombi maalam kwa malaika wa mbinguni ni sawa kibiblia? Kwa mfano; kumuomba malaika wako mlinzi akulinde asubuhi unapoamka au sala kwa mtakatifu Mikaeli malaika mkuu, au rozari ya malaika mkuu mikaeli n.k je! Hayo ni sawa kimaandiko?


JIBU: Si sawa kimaandiko hata kidogo. Kumekuwa na mafundisho ambayo yanafundisha watu kufanya sala au maombi kwa malaika fulani, mfano; kuna watu wanafundisha mafundisho ya rozali ya malaika mkuu mikaeli na kusema kuwa sala hii ni nzuri sana ya kumuheshimu huyo malaika mkuu mikaeli na makundi yote tisa ya malaika mbinguni kwa sababu malaika mikaeli alimtokea mtakatifu fulani na kumfundisha sala hii, ndugu yangu, nataka nikwambie kuwa, huyo mtakatifu wako alitokewa na shatani na wala si malaika, kwa sababu shetani pia anaweza kujigeuza na kujifanya kuwa malaika wa nuru.


2 Wakorinto 11:14  Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. 


Hupaswi kumwomba malaika yoyote yule akulinde, ama kwa sara, au rosali, unapo fanya hivyo fahamu kuwa, unayaomba mapepo hapo na wala sio malaika (kwa sababu malaika wa Bwana hawaombwi) unayetakiwa kumwomba ulinzi na mambo mengine yote ni Bwana peke yake (Yohana 14:14) Malaika ni roho zitumikazo kuwahidumia wale watakaourithi ufalme.


Waebrania 1:13 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?

14 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu? 


Viongozi wengi vipofu wanafundisha watu mambo kama hayo ambayo yapo kinyume kabisa na imani ya Kikristo bila kuchunguza kama wanayofundisha yapo sawa na mafundisho ya mitume au la! Wengi walifundishwa kutoka kwa viongozi wao vipofu, ambao nao pia walifundishwa kutoka kwa viongozi wao vipofu, ambao nao pia wali-copy kutoka kwa viongozi wao vipofu, ambao mwisho wao wote ni kutumbukia shimoni kama wasipotaka kureje katika mafundisho ya mitume.


Matayo 15:14 Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili. 


Ndugu unayesoma ujumbe huu fahamu kuwa, hakuna sala wala maombi kwa ajili ya malaika fulani (awe Mikaeli au Gabriel) hao wote wanatumwa na Bwana katika utumishi  ikiwemo na kuwatumikia wanadamu.

Hata mtume Yohana alipoanguka mbele ya yule malaika ili amwabudu, malaika alimwambia usifanye hivi.


Ufunuo 19:10  Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, USIFANYE HIVI; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii. 


Sasa wewe huyo mtakatifu wako alitolewa na malaika gani aliyemfundisha mambo yaliyopo kinyume na neno la Mungu? Huyo malaika atakuwa amelaaniwa na wala sio wa Mungu ila wa shetani. Hivyo acha mara kufanya hivyo, umgeukie Kristo na kutubu dhambi zako kisha kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu atakayekutia katika kweli yote na kukufanya uyaishi mapenzi ya Mungu.


Ikiwa utakuwa na swali lolote kuhusu biblia, basi, wasiliana nasi kwa namba hizi

+255652274252/ +255789001312

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu

Bwana akubariki, shalom.


MADA ZINGINEZO:

Mailaika mikaeli ndiye Bwana Yesu?


Nini maana ya wanawake saba watamshika mume mmoja?( Isaya 4:1)


Waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi. 



Pazia la Hekalu ni nini katika biblia?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *