SWALI: je! Ni sahihi kwa Mkristo kwenda kwenye makabauri au mapango na kuwaomba au kuwauliza mababu zake waliofariki zamani?
JIBU: Hapana! Si sawa hata kidogo kwa Mkristo kwenda kwenye makaburi na kuwaomba au kuuliza jambo huko kwa mabubu zake waliofariki tangu zamani kwani maandiko ya Roho Mtakatifu yanakataza kuomba na kuuliza chochote kwa watu waliokufa wakiwemo na mababu zetu.
Isaya 8:19 Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? JE! WAENDE KWA WATU WALIOKUFA KWA AJILI YA WATU WALIO HAI?
Kumekuwa na baadhi ya mila na tamaduni ambazo huamini kuwa, kuna mizimu ya mababu katika makaburi au mapango na katika matambiko, ambayo yanaweza saidia tatizo endapo yakiulizwa na kuombwa. Na baadhi ya watu wanashuhudia kuwa ni Kweli na kuna vitu wanaviomba na vinafanyika. Lakini nataka nikwambie wewe Mkristo kuwa, hao sio mababu zako kama unavyodhani, bali ni mapepo unayoyauliza na kuyaomba ambayo yanatumia kivuli cha mababu zako kukudanganya, na wala sio hao tu, lakini pia kitendo hicho kinafanywa na dhehebu la kanisa katoliki, ambalo katika mafundisho yao baadhi wanaamini kuwa, ukichukua udongo kutoka kwenye kaburi la marehemu (mtakatifu) fulani unaweza pata msaada fulani wa kiroho kitu ambacho ni mafundisho potofu kutoka kwa mwovu, kama ulikuwa huko toka na ugeukie injili ya kweli ya Yesu Kristo kwa kutubu dhambi zako na kubatizwa kwa jina lake.
Hivyo, kama wewe ni mkristo na umeshampa Kristo maisha yako na kuigeukia nuru, hupaswi kwenda na kuwaomba mababu zako hata kama ni utamaduni wenu, acha mara moja kwa sababu injili ya Kristo ilihubiriwa kwako ili ikutoe katika hizo nguvu za shetani na mapepo yanayojifanya kuwa ni mababu zako.
Matendo Ya Mitume 26:16 Lakini inuka, usimame kwa miguu yako, MAANA NIMEKUTOKEA KWA SABABU HII, NIKUWEKE WEWE UWE MTUMISHI NA SHAHIDI WA MAMBO HAYA ULIYOYAONA, na wa mambo ambayo katika hayo nitajidhihirisha kwako;
17 nikikuokoa na watu wako, NA WATU WA MATAIFA, AMBAO NAKUTUMA KWAO;
18 UWAFUMBUE MACHO YAO, NA KUWAGEUZA WAIACHE GIZA NA KUIELEKEA NURU, WAZIACHE NA NGUVU ZA SHETANI na kumwelekea Mungu; KISHA WAPATE MSAMAHA WA DHAMBI ZAO, NA URITHI MIONGONI MWAO WALIOTAKASWA KWA IMANI ILIYO KWANNGU MIMI.
Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.
Bwana akubariki, Shalom.
+255652274252/ +255789001312
Mada zinginezo:
Maziwa ya akili yasiyoghoshiwa ni yapi, kibiblia?(1Petro 2:2)
Je! Ni dhambi kibiblia kuwaomba wafu (watakatifu)?
Biblia imeruhusu ubatizo wa vichanga? (kulingana na matendo 16:33)
Bwana wa mavuno ni nani? (Mathayo 9:38)
Hongereni kwa kutoa mafundisho na kutuongoza kwenye kweli.
Ubarikiwe sana ndugu yetu, Utukufu kwa Bwana.